Ofisa Mahusiano Wateja Binafsi wa benki ya CBA, Rosemary Ihadike (kulia), akimpatia maelezo, mgeni rasmi katika uzinduzi wa maonesho ya ya Sekta ya Nyumba Tanzania, (Tanzania Homes Expo 2012), Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yussuf Mwenda, wakati alipokuwa akitembelea mabanda mbalimbali kwenye maonesho hayo, kabla ya kuyazindua, viwanja vya Mlimani City, Dar es Salaam leo. Wengine katikati ni baadhi ya Maofisa wa benki hiyo, Halima Hussein na Anitha.
Mchambuzi wa Viwango katika Maabara wa Kampuni ya Simba Cement, Charles Mbelwa, akimpatia maelezo mgeni rasmi katika uzinduzi wa maonesho ya ya Sekta ya Nyumba Tanzania, (Tanzania Homes Expo 2012), Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yussuf Mwenda, kuhusu ubora wa bidhaa za kiwanda hicho zinavyopatikana (kwenye chupa) kabla ya kutengenezwa kibiashara kiwandani, wakati Meya huyo, alipotembelea banda la kampuni hiyo, kwenye maonesho hayo kabla ya kuyazindua, viwanja vya Mlimani City, Dar es Salaam leo.
Mwqenyekiti wa Kampuni ya Landmarks, Rustam Merani (kushoto), akimpatia kipeperushi chenya maelezo ya kampuni yake, mgeni rasmi katika uzinduzi wa maonesho ya Sekta ya Nyumba Tanzania, (Tanzania Homes Expo 2012), Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yussuf Mwenda, wakati alipokuwa akitembelea mabanda mbalimbali kwenye maonesho hayo, kabla ya kuyazindua, viwanja vya Mlimani City, Dar es Salaam leo.
Meneja wa Tawi la Dar es Salaam wa Kampuni ya kuchonga miamba ya Marmo & Granito Mines Tanzania, Imran Jessa, akimpatia maelezo kuhusu bidhaa zinazo zalishwa na kiwanda cha kampuni hiyo, mgeni rasmi katika uzinduzi wa maonesho ya Sekta ya Nyumba Tanzania, (Tanzania Homes Expo 2012), Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yussuf Mwenda (kulia), wakati alipokuwa akitembelea mabanda mbalimbali kwenye maonesho hayo, kabla ya kuyazindua jijini leo. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Maonesho, Zeno Ngowi.
Mratibu wa Kitengo cha Huduma kwa wateja wa benki ya KCB, Shose Kombe, akimweleza mgeni rasmi katika uzinduzi wa maonesho ya Sekta ya Nyumba Tanzania, (Tanzania Homes Expo 2012), Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yussuf Mwenda, kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo nchini, wakati alipokuwa akitembelea mabanda mbalimbali kwenye maonesho hayo, kabla ya kuyazindua, viwanja vya Mlimani City, Dar es Salaam leo. Katikati ni Ofisa Mauzo wa KCB, Himid Rashid.
Ofisa Mahusiano wa Benki ya KCB, Christopher Mmbaga (wa pili kulia), akiwapatia maelezo ya huduma zitolewazo na benki hiyo, wakati walipotembelea banda lao, kwenye maonesho ya Sekta ya Nyumba Tanzania, (Tanzania Homes Expo 2012), viwanja vya Mlimani City, Dar es Salaam leo. Kulia ni Mratibu wa Kitengo cha Huduma kwa wateja wa KCB, Shose Kombe.
Ofisa Mikopo wa benki ya Exim, Hosiana Muro (kulia), akimpatia maelezo, mgeni rasmi katika uzinduzi wa maonesho ya Sekta ya Nyumba Tanzania, (Tanzania Homes Expo 2012), Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yussuf Mwenda, wakati alipokuwa akitembelea mabanda mbalimbali kwenye maonesho hayo, viwanja vya Mlimani City, Dar es Salaam leo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Global Land Solutions, Murtaza Adamjee (wa pili kulia), akimpatia maelezo, mgeni rasmi katika uzinduzi wa maonesho ya Sekta ya Nyumba Tanzania, (Tanzania Homes Expo 2012), Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yussuf Mwenda, kuhusu michoro ya majumba yao ya kibiashara, yaliyopo Jangwani Beach Mbezi jijini Dar es Salaam, wakati alipokuwa akitembelea mabanda mbalimbali kwenye maonesho hayo, kabla ya kuyazindua, viwanja vya Mlimani City, Dar es Salaam leo.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa Maonesho ya Sekta ya Nyumba Tanzania, (Tanzania Homes Expo 2012), Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yussuf Mwenda, akikata utepe kwa pamoja na Mkurugenzi wa Maonesho hayo, Zeno Ngowi (kushoto), ili kuyazindua maonesho hayo, Viwanja vya Mlimani City, Dar es Salaam leo. Maonesho hayo yanafungwa kesho na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk. Mohamed Gharib Bilal.
Mkurugenzi wa Maonesho ya Sekta ya Nyumba Tanzania, (Tanzania Homes Expo), Zeno Ngowi, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati wa ufunguzi wa maonesho Viwanja vya Mlimani City jijini.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa Maonesho ya Sekta ya Nyumba Tanzania, (Tanzania Homes Expo 2012), Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yussuf Mwenda, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, mara baada ya kuyafungua maonesho hayo, Viwanja vya Mlimani City jijini. Kushoto ni Mkurugenzi wa Maonesho hayo, Zeno Ngowi.
No comments:
Post a Comment