Meneja wa kitengo cha uchambuzi wa mifumo ya kompyuta kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Mwanaidi Mahiza, akitoa elimu ya uhifadhi na utunzaji wa karatasi za madodoso ya Sensa ya watu na makazi 2012 kwa waratibu wa Sensa kutoka mikoa na wilaya zote nchini katika mafunzo ya awali yanayoendelea mjini Morogoro.
Waratibu wa Sensa ya watu na Makazi 2012, kutoka katika Mikoa na Wilaya zote nchini wakifuatilia mada mbalimbali kutoka kwa wataalam wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, mjini Morogoro. Katika mkutano huo wa mafunzo, mambo mbalimbali yamejadiliwa, yakiwemo masuala ya Bajeti, Ushiriki wa Viongozi katika zozi la Sensa, Utunzaji na ujazaji wa madodoso wakati wa Sensa, namna ya kuwapata makarani wa Sensa na vitendea kazi.
Waratibu wa Sensa ya watu na makazi, wakipitia moja ya dodoso litakalotumika wakati wa Sensa ya watu na makazi mwezi Agosti mwaka huu na kujifunza namna sahihi ya kuweka vivuli/ alama wakati wa kukusanya taarifa za kaya.
Viongozi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bara na ile ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, viongozi wa Mkoa wa Morogoro na waratibu wa Sensa ya watu na makazi 2012, wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Alphayo Kidata (mstari wa mbele katikati), mjini Morogoro. (Picha zote na Aron Msigwa - MAELEZO.)
No comments:
Post a Comment