TANGAZO


Tuesday, June 5, 2012

Nape aingia Njombe kuimarisha Chama, kukagua miradi ya maendeleo

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye  akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mlangali, wilayani Ludewa, mkoani Njombe, akiwa katika ziara ya kuimarisha uhai wa Chama na kukagua miradi ya maendeleo mkoani humo jana.



Nape akiwahutubia wananchi katika kijiji cha  Mlangali, wilayani Ludewa mkoani Njombe akiwa katika ziara ya kuimarisha uhai wa chama mkoani wilayani humo, jana.

Wanachi wakiwa wamekaa juu ya mbao ili kuweza kumuona vizuri Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye, wakati alipokuwa akiwahutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mlangali, mkoani Njombe jana.



Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye  akipiga ngoma, wakati wa mapokezi yake katika kijiji cha Mlangali mkoani Njombe jana 4/6/2012.


Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye  akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadahara, uliofanyika katika Uwanja wa Turbo, mjini Njombe, akiwa katika ziara ya kuimarisha uhai wa Chama na kukagua miradi ya maendeleo mkoani humo, leo 5/6/2012.


Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye  akihutubia wananchi katika mkutano huo wa hadahara, uliofanyika Uwanja wa Turbo, mjini Njombe leo, akiwa katika ziara ya kuimarisha uhai wa Chama na kukagua miradi ya maendeleo mkoani humo.

Mama aliyebeba mtoto, akishangilia kwa furaha wakati wa uzinduzi wa tawi la wakereketwa wa CCM la Liwigi, Ludewa mkoani Njombe uliofanyuwa na Nape Nnauye katika ziara hiyo.


Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, akifurahi na watoto wa Mlangali, alipopiga nao picha ya pamoja na watoto hao baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara eneo hilo.


Msafara wa Nape ukiongozwa na pikipiki wakati ukiingia mjini Njombe kwa ajili ya mkutano wa hadhara na kufungua matawi kadhaa ya CCM. 

Msafara wa Nape ukiwa magari na pikipiki wakati ukiingia mjini Njombe kwa ajili ya mkutano wa hadhara na kufungua matawi ya CCM. 

Nape akimbeba mtoto  Goodluck John wa shule ya awali ya Lutheran, iliyopo Melizine nje kidogo ya mji wa Njombe, baada ya kumkuta mtoto huyo akiwa na wanafunzi wenzake miongoni mwa watu waliokuwa wakisubiri msafara wake kupita eneo hilo akiwa njiani kuingia mjini Njombe.

Nape akizindua shina la wakereketwa wa CCM la Melizine mjini Njombe wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa Chama mkoani Njombe.

Wanafunzi wa shule ya awali ya Melizine wakionyesha alama ya dole, wakati Nape alipopita eneo la shule yao mjini Njombe  leo 5/6/12. (Picha zote na Bashir Nkoromo)

No comments:

Post a Comment