Baadhi ya wananchi wa eneo hilo, wakiwa wameyazunguka magari la Polisi, wakati walipofika kujaribu kuwaondoa kwenye eneo hilo ili kupisha magari yaweze kupita kama kawaida.
Baadhi ya magari yaliyoshindwa kupita kwenye eneo hilo, yakitokea Gongolamboto kuelekea mjini na kusababisha msururu mrefu wa magari hayo.
Baadhi ya magari yaliyoshindwa kupita kwenye eneo hilo, kutokana na kadhia hiyo leo Juni 12, 2012, yakitokea mjini kuelekea Gongolamboto.
Baadhi ya wananchi wa eneo la Majumba Sita, Ukonga Dar es Salaam, wakiwa wemefunga barabara ya eneo hilo huku magari ya Polisi yakiwa yamewekwa kati baada ya kufika kwenye eneo hilo na kujaribu kuwashawishi wananchi hao kuondoka, hatua waliyoikata, wakidai kwanza kufika Mkuu wa Mkoa, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala ama Mkurugenzi wa TANROAD.
Vijana wakiwa wameinua bango lililokuwa na ujumbe kwa Serikali wa kuitaka kuwajengea matuta kwenye sehemu hiyo ya Majumbasita.
Kijana wa kike, aliyejitambulisha kwa jina la Subira Mohamed, akiwa amenyanyua bango lenya ujumbe usemao "Tunamtaka Mkuu wa Mkoa aje leo", wakati walipokuwa wamefungwa barabara hiyo leo.
Mmoja wa maofisa wa jeshi la Polisi, aliyetambulika kwa jina moja tu la Mambosasa, akijaribu kuwaomba wananchi wa Majumba Sita, Ukonga Dar es Salaam kuondoka barabarani ili kuruhusu magari kupita baada ya kuyazuia kwa zaidi ya saa 3, kuishinikiza Serikali kuwawekea matuta katika barabara hiyo inayotoka Gongolamboto kuelekea mjini, kutokana na ajali zinazotokea kwenye eneo hilo.
Mambosasa, akiendelea kuwanasihi wananchi wa Majumba Sita, kuondoka kwenye eneo la barabara hiyo ili kuruhusu magari kuendelea kupita lakini hakuweza kufanikiwa hadi pale alipowaahidi kuondoka na wawakilishi wao kwenda kunakohusika kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi tatizo lao hilo.
Wawakilishi wa wananchi, kutoka kushoto kwenye gari la Polisi ni Jamhuri Saleh, Mboni Idd na Ester Mushi, wakiwa tayari kuondoka na gari hilo kwenda kufuatilia ufumbuzi wa tatizo lao hilo, hatua iliyokubaliwa na wakazi wa eneo hilo na kuondoka barabarani kupisha magari kuendelea kupita kama kawaida.
No comments:
Post a Comment