TANGAZO


Tuesday, June 12, 2012

Odinga ataka EU kuwashambulia al-shabab

Rais Kibaki na Waziri Mkuu Odinga-Kenya imeomba msaada kupambana na al-shabab
Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga ameomba msaada kifedha na vikosi kutoka Marekani na Ulaya kuwatoa al-Shabab kwa ‘shambulio la mwisho’ katika mji wenye bandari wa Kismayo.
Raila Odinga alisema vikosi vyaKenya vinatarajia kuingia Kismayo mwezi Agosti na alisema al-Shabab itahitaji "operesheni ya kivita ardhini, baharini na angani".
Lakini msemaji wa sera za nje wa Muungano wa Ulaya Michael Mann alisema hiyo ni kwenda kinyume na majukumu yake.
Manowari za kivita zimekuwa katika eneo hilo tangu mwaka 2008 kupambana na maharamia.
Majukumu yake hivi karibuni yaliongezeka ili kuruhusu mashambulizi ya ardhini dhidi maharamia wa Kisomali.
Hadi manowari kumi za kivita zinafanya doria katika Pembe ya Afrika kama sehemu ya harakati ya Muungano wa Ulaya ‘Atalanta’ ambayo ilianzishwa kulinda biashara za bandarini dhidi ya mashambulizi ya maharamia.
Lakini Bw Mann aliiambia BBC: "Hatuna budi kuwa makini sana kufanya harakati zetu katika mzingo wa sheria za kimataifa. Tunawajibika katika jukumu letu ambalo ni kupambana na maharamia baharini kwa kuharibu mgome zao.
"Iwapo tutabadili hilo tutahitaji nchi wanachama 27 kukubaliana na hilo. Kwa sasa tunaona kuwa kupambana na al-Shabab kwa ufanisi zaidi hakuna budi kufanywe kwa namna nyingine"

'Kuwamaliza al-Shabab'

Askari wa Umoja wa Afrika, vikosi vya Ethipia na vile vya serikali ya mpito yaSomalia katika miezi ya karibuni yamefanikiwa kuwaondoa al-shabab katika miji kadhaa.
Vikosi vya Kenya viliingia Somalia mwezi Oktaba mwaka jana na taratibu vinasogea kuelekea Kismayo.
Kismayo kimsingi inachukuliwa kama mji muhimu wapiganaji wa al-Shabab kwa sababu wanaudhibiti kupata fedha kutokana na mapato na kodi katika bandari hiyo.

No comments:

Post a Comment