Waislamu wakiwa kwenye maandamano, Viwanja vya Kidongo Chekundu, Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo, kumshinikiza Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dk. Joyce Ndalichako kujiuzulu kutokana na kile wanachodai kuhujumiwa kwa wanafunzi wa Kiislamu kwenye mitihani inayosimamiwa na Baraza hilo, chini ya Uongozi wa Dk. Ndalichako.
Mmoja wa waandamanaji hao, akionesha bango lenye kutaka Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), kuvunjwa wakati wa maandamano yao hayo, Viwanja vya Kidongo Chekundu, Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya Waislamu hao, wakinyanyua juu mabango yaliyokuwa yakimweleza Rais Jakaya Kikwete kuchoshwa kwao na hila za viongozi wa Baraza hilo.
Baadhi ya Waislamu hao, wakinyanyua juu mabango yaliyokuwa na ujumbe mbalimbali kuhusu kutokutendewa haki kwa wanafunzi wa Kiislamu na mengine yakimtaka Katibu huyo kujiuzulu kwenye Baraza hilo.
Baadhi ya Waislamu hao, wakiwa wamenyanyua juu mabango yaliyokuwa na ujumbe mbalimbali, mengine yakimtaka Dk. Ndalichako kujiuzulu, mengine kulitaka Baraza hilo kuacha kuwafelisha wanafunzi wa Kiislamu na mengineyo mengi.
Baadhi ya Viongozi wa Kiislamu kwenye maandamano hayo, kutoka kushoto, Ustaadhi Kondo Bungo, Ustaadhi Seleman Daud (katikati anayeongea) na Shaaban Mapeyo,wakipiga Takbir kwenye maandamano hayo.
Baadhi ya Viongozi wa Kiislamu kwenye maandamano hayo, kutoka kushoto, Ustaadhi Kondo Bungo, Ustaadhi Seleman Daud (katikati) na Shaaban Mapeyo, wakiongea na waandishi wa habari kwenye maandamano hayo, Viwanja vya Kidongo Chekundu, Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu, Sheikh Issa Ponda, akizungumza na Waislamu wakati walipokuwa kwenye maandamano hayo, Viwanja vya Kidongo Chekundu, Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo, kushinikiza Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dk. Joyce Ndalichako, kujiuzulu nafasi yake.
Baadhi ya Viongozi wa Kiislamu kwenye maandamano hayo, wakielekea kwenye gari la Polisi (kulia), kwa ajili ya kwenda Wizara ya Elimu kuwasilisha ujumbe wao kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, baada ya kuzungumza na Polisi na kuelewana kufanya hivyo, ili kuepuka uwingi wa watu kwenye eneo la Wizara na pia barabarani, ambako yangelipita maandamano hayo.
Baadhi ya Viongozi wa Kiislamu kwenye maandamano hayo, wakipanda kwenye gari la Polisi (kulia), kwa ajili ya kwenda Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kuwasilisha ujumbe wao kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Shukuru Kawambwa.
Viongozi hao wa Kiislamu kwenye maandamano hayo, wakipanda gari la Polisi kwa ajili ya kwenda Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi, kuwasilisha ujumbe wao kwa Waziri Shukuru Kawambwa.
Viongozi wa Kiislamu katika maandamano hayo, wakiondoka na gari la Polisi, kuelekea Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa ajili ya kwenda kwa Waziri Kawambwa, kuwasilisha ujumbe wao huo, huku wakiungwa mkono na wafuasi wao. (Picha zote na Dotto Mwaibale)
No comments:
Post a Comment