Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi 'SUGU', akibadilishana mawazo na Mbunge mwenzake kutoka Jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe (kushoto) katika viwanja vya Bunge leo, wakati wa mapumziko ya mchana ya Bunge la Bajeti linaloendelea mjini Dodoma.
Mbunge wa Mbeya Mjini joseph Mbilinyi 'SUGU', na Mbunge mwenzake kutoka Jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe (kushoto), wakifahamishana jambo, wakati wa mapumziko ya mchana ya Bunge la Bajeti linaloendelea mjini Dodoma leo.
Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda (kulia), akibadilishana mawazo na Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka leo, wakati wa mapumziko ya mchana ya kikao cha Bunge cha Bajeti, linaloendelea mjini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda (katikati), akibadilishana mawazo na Wabunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka (kushoto) na wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela,wakati wa mapumziko ya mchana ya kikao cha Bunge la bajeti linaloendelea mjini Dodoma leo.
Baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakijaza fomu za vitambulisho vya Taifa (NIDA), leo katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma. (Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO-Dodoma)
No comments:
Post a Comment