TANGAZO


Friday, June 22, 2012

Stika zenye namba za simu za vituo vya Polisi kubandikwa sehemu mbalimbali jijini


 Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani, Mohamed Mpinga (katikati), akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua kampeni ya kubandika stika zenye namba za simu za vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam leo, ambazo abiria watazitumia kwa ajili ya kutoa taarifa za usalama na matukio ya uvunjifu wa sheria barabarani. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), wadhamini wa kampeni hiyo, Sabasaba Moshingi. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi, akibandika moja ya sitika hizo ndani ya daladala.
Mmoja wa madereva wa daladala, waliokabidhiwa Stika hizo kwa ajili ya kuzibandika kwenye magari, akiwaonesha waandishi wa habari waliokuwepo katika uzinduzi wa kampeni hiyo, inayodhaminiwa na benki ya Posta Tanzania (TPB), jijini leo. (Picha na Mdau wetu)

No comments:

Post a Comment