TANGAZO


Friday, June 22, 2012

Airtel yakabidhi vifaa vya michezo kwa shule za msingi za Mwangaza, Maarifa na Gongolamboto Jaika

Afisa uhusiano wa Airtel, Jane Matinde, akikabidhi jezi za mpira kwa Mwalimu
wa Taaluma na michezo wa Shule ya Msingi ya Gongolamboto Jaika leo. Mwl. Almasi
Shemdoe wakati Airtel, ilipotembelea Shule za Msingi za Gongolamboto za
Mwangaza, Maarifa na Gongolamboto Jaika Dar es Salaam na kugawa vifaa vya michezo.

Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde, akikabidhi jezi za mpira wa miguu kwa  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Maarifa. Mwalimu Marietha Mulyalya, wakati Airtel ilipotembelea Shule za  Mwangaza, Maarifa na Gongolamboto Jaika, Gongolamboto jijini Dar es Salaam na kukabidhi vifaa vya michezo leo.

Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde, akikabidhi jezi za mpira wa miguu kwa  Mwalimu wa Taaluma na michezo wa Shule Msingi ya Mwangaza, Mwalimu Abdul Mwarami, wakati Airtel ilipotembelea Shule za Msingi za Mwangaza, Maarifa na Gongolamboto Jaika, Gongolamboto Dar es Salaam leo na kukabidhi vifaa vya michezo. 



Walimu wa shule za msingi za Mwangaza, Maarifa na Gongolamboto Jaika, wakiwa na jezi zao mara baada ya kukabidhiwa vifaa vya michezo na Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel, makabidhiano hayo yalifanyika katika shule ya Msingi Maarifa Gongolamboto jijini  Dar es Saalam leo. Pichani katikati ni Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde. 

Walimu wa shule za msingi za Mwangaza, Maarifa na Gongolamboto Jaika, wakifurahia jezi zao, huku wakizionesha kwa waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa vifaa vya michezo na Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel, makabidhiano hayo yalifanyika katika Shule ya Msingi Maarifa Gongolamboto jijini  Dar es Saalam leo. Pichani katikati ni Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde. (Picha na Mdau wetu)


No comments:

Post a Comment