TANGAZO


Friday, June 22, 2012

Mbunge Zungu akabidhi pikipiki kwa kikundi cha ushirika cha Dizonga, Ilala Bungoni

 Diwani wa Kata ya Ilala (viti maalum), Tumike Malilo, akiijaribu kuiwasha pikipiki iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan 'Zungu' kwa kikundi cha ushirika wa Mfuko wa Maendeleo Dizonga cha mtaa wa Mafuriko, Ilala Bungoni, kabla Diwani wa Kata hiyo, Edson Fungo (wa tatu kulia), kuikabidhi kwa Mwenyekiti wa kikundi hicho, Ramadhan Juma (wa pili kulia aliyefichika), Dar es Salaam jana. Kulia ni Mjumbe wa Serikali ya mtaa huo, Ally Mshauri. (Picha zote na Kassim Mbarouk)


 Diwani wa Kata ya Ilala (viti maalum), Tumike Malilo, akifurahia pikipiki hiyo baada ya kuiwasha, pikipiki iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan 'Zungu' kwa kikundi cha ushirika wa Mfuko wa Maendeleo Dizonga cha mtaa wa Mafuriko, Ilala Bungoni, kabla Diwani wa Kata hiyo, Edson Fungo (katikati mwenye shati jeupe), kuikabidhi kwa kikundi hicho, Dar es Salaam jana. Kulia ni Mjumbe wa Serikali ya mtaa huo, Ally Mshauri. 


 Mwenyekiti wa kikundi hicho, Ramadhan Juma, akiipinda pikipiki hiyo, ili kuijaribu baada ya kukabidhiwa na Diwani wa Kata ya Ilala, Edson Fungo (katikati) wa Kata ya Ilala kwa niaba ya Mbunge Mussa Azzan 'Zungu', ambaye yuko Bungeni mjini Dodoma.


 Diwani wa Kata hiyo, Edson Fungo (katikati), akizungumza na wanakikundi cha Ushirika huo, mara baada ya kuwakabidhi pikipiki hiyo jana. Kulia ni Diwani wa Kata ya Ilala (viti maalum), Tumike Malilo.


Diwani wa Kata ya Ilala (viti maalum), Tumike Malilo, akizungumza na wanakikundi cha ushirika wa Mfuko wa Maendeleo Dizonga cha mtaa wa Mafuriko, Ilala Bungoni, mara baada  Diwani wa Kata hiyo, Edson Fungo (katikati), kukabidhi pikipiki iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan 'Zungu' kwa kikundi cha kwa Mwenyekiti wa kikundi hicho, Ramadhan Juma (kushoto juu ya pikipiki), Dar es Salaam jana. 

No comments:

Post a Comment