Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira Endelevu (Rio+20) jana Juni 21, jijini Rio de Janeiro, nchini Brazil jana.
Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Fatma Fereji, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Terezya Huvisa, wakiwa katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira Endelevu (Rio+20) jana Juni 21, jijini Rio de Janeiro, nchini Brazil.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Terezya Huvisa (katikati), Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Fatma Fereji na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim (kulia nyuma), wakiwa katika Ukumbi wa mkutano, wakati walipohudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira Endelevu (Rio+20) jana Juni 21, jijini Rio de Janeiro, nchini Brazil.
Balozi Liberata Mulamula (kulia) na Balozi wa Tanzania, nchini Brazil, Francis Malambugi (wa pili mstari wa mbele), wakiwa katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira Endelevu (Rio+20) jana Juni 21, jijini Rio de Janeiro, nchini Brazil. Mkutano huo ni wa pili kufanyika nchini hapa tangu ulipofanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1992.
No comments:
Post a Comment