Baadhi ndugu wa marehemu Willy Edward, wakiangua vilio baada mwili kuwasili nyumbani kwao Mugumu, Serengeti jana usiku. Mwili huo unazikwa kesho nyumbani kwao hapo.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Willy Edward, likiingizwa ndani baada ya kuwasili nyumbani kwao Mjini Mugumu, wilayani Seerengeti jana usiku.
Mjane wa marehemu Willy Edward Rehema, akilia kwa uchungu juu ya jeneza la mumewe baada ya mwili wake kuwasili nyumbani kwao Mjini Mugumu jana usiku.
Baadhi ndugu wa marehemu Willy Edward, wakiangua vilio mbele ya jeneza.
Mmoja wa waombolezaji akisoma habari za kifo cha aliyekuwa Mhariri Mkuu wa Jambo leo, marehemu Willy Edward wakati wa shughuli za msiba mjini Mugumu, wilayani Serengeti leo.
Mzee Edward Ogunde, baba wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward akifarijiwa na mwakilishi wa Kampuni ya Jambo Concepts Limited, inayochapisha gazeti la Jambo Leo na Jarida la Jambo Brand Tanzania, Anicetus Mwesa nyumbani kwao marehemu, Mugumu Mjini, wilayani Serengeti leo. Willy anazikwa kesho eneo la nyumba yao karibu na kaburi la mamake. Katikati ni mdogo wa marehemu, Essey Ogunde.
Mmoja wa waombolezaji Noah Ongiri, akitumbuiza kwa kutumia kipaza sauti, alichojitengenezea wakati wa msiba wa mpendwa wao marehemu Willy Edward. (Picha zote na Richard Mwaikenda)
No comments:
Post a Comment