Bondia Ramadhani Shauri akiwa ameushika mkanda wa I.B.F Africa, wakati ulipokuwa ukiuonesha mbele ya waandishi wa habari baada ya kuwasili Dar es salaam jana, akitokea nchini Marekani (USA). Mkanda huo utakaogombaniwa na Shauri kwa kupambana na Sande Kizito wa Uganda katika mpambano utakaofanyika siku ya Iddi pili, ukumbi wa Diamond Jubilee jijini. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), Madaraka Nyerere na Promota wa mpambano huo, Mkurugenzi wa Kitwe General Traders, Lucas Rutainirwa (Picha zote na Super D, Mnyamwezi)
Bondia Nassibu Ramadhani (kushoto) na Ramadhani Shauri, wakiufungua mkanda wa ubingwa wa IBF Africa, utakaogombaniwa na Ramadhani Shauri (wa pili kulia) na bondia Sande Kizito wa Uganda.
Ramadhani Shauli akiwa na mkanda wa ubingwa wa IBF Africa, Dar es Salaam jana.
No comments:
Post a Comment