Alisher Usmanov
Tajiri mmoja anayemiliki kiasi kikubwa katika hisa za klabu
ya Arsenal, Alisher Usmanov anasema angependa kununua hisa zaidi za klabu hio
ingawa hana nia ya kupata nafasi kwenye bodi inayoongoza klabu.
Usmanov ambaye ndiye tajiri mwenye vipesa kuliko tajiri mwingine nchini jimbo
la zamani la Urussi la Uzbekistan, ni mmoja wa matajiri kadhaa wanaomiliki hisa
katika klabu za Uingereza kama Roman Abramovich huko Chelsea na Anton
Zingarevich wa Reading.
Arsenal fc
Usmanov ameliambia shirika la habari la Reuters nje ya mji wa Petersburg kua
'daima na kwa kiwango chochote, nipo tayari kuongezea kiwango cha hisa
zangu.
Usmanov, ambaye utajiri wake umetokana na biashara ya chuma na teknolojia
anaweza kujijengea umaarufu na nafasi kwenye bodi kutokana na kiwango cha hisa
atakazowekeza.Chombo cha Red and White, kinachomilikiwa na Usmanov kwa ushirikiano na Farhad Moshiri,wana miliki asili mia 29.72 ya hisa katika Arsenal,kwa mujibu wa Tovuti ya klabu hio.
Stan Kroenke
Kwa mujibu wa habari za vyombo vya habari mmiliki mkubwa wa hisa za Arsenal, Kroenke anachukizwa kusikia kama Usmanov angepewa nafasi kwenye bodi ya Arsenal.
No comments:
Post a Comment