TANGAZO


Wednesday, June 13, 2012

Wabunge wakibadilishana mawazo nje ya ukumbi wa Bunge, Dodoma leo


Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto), Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makalla (katikati) na Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Anna Abdallah wakibadishana mawazo leo, nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma mara baada ya kipindi cha maswali na majibu ya kikao cha pili cha Mkutano wa nane wa Bunge kumalizika. (Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dodoma)

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia, wakibadishana mawazo nje ya ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Dk. Milton Makongoro Mahanga leo, mara baada ya kipindi cha maswali na majibu ya kikao cha pili cha Mkutano wa nane wa Bunge kumalizika.


Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara na Naibu wake, Amos Makalla, wakijadiliana jambo leo nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, mara baada ya kipindi cha maswali na majibu ya kikao cha pili cha Mkutano wa nane wa Bunge kumalizika.



Naibu Spika wa bunge la Tanzania Job Ndugai (kushoto), akiwa na Mbunge wa Iramba Mashariki Mwigulu Nchemba, wakibadilishana mawazo nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo, mara baada ya kipindi cha maswali na majibu ya kikao cha pili cha Mkutano wa nane wa Bunge kumalizika.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Mwita Werema (kulia) na Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila, wakibadilishana mawazo nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo, mara baada ya kipindi cha maswali na majibu kumalizika.


Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Milton Makongoro Mahanga na Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum, wakijadiliana jambo nje ya ukumbi wa Bunge, mara baada ya kipindi cha maswali na mjibu kumalizika  mjini Dodoma leo.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika (kulia), akijadiliana jambo leo nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma na Mbunge wa Jimbo la Tanga, Omar Nundu mara baada ya kipindi cha maswali na majibu ya kikao cha pili cha Mkutano wa nane wa Bunge kumalizika.

Mbunge wa Tabora mjini, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Simba Sport Club, Ismail Aden Rage (kushoto) akibadilishana mawazo na Naibu Waziri wa Maji, Dk. Binilith Satano Mahenge leo, nje ya ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma mara baada ya kipindi cha maswali na majibu kumalizika.


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Gregory Teu (kushoto), akibadilishana mawazo na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai leo, nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma mara baada ya kipindi cha maswali na majibu kumalizika.


Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali na pia Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo (kulia), Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba (katikati) na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, wakibadishana mawazo leo, nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma mara baada ya kipindi cha maswali na majibu ya kikao cha pili cha Mkutano wa nane wa Bunge kumalizika.

No comments:

Post a Comment