TANGAZO


Wednesday, June 6, 2012

Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wala Kiapo


Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki leo wamekula kiapo cha kulitumikia bunge hilo jijini Arusha.

Wabunge waliokula kiapo kutoka Tanzani  leo hii ni pamoja na Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania kwenye Bunge la Afrika ya Mashariki (EALA), Alhaj Adam Omar Kimbisa na Katibu wake, Shy-Rose SaddrudinBhanji.

Wengine ni Anjela Charless Kizigha, Maryam Ussi Yahya, Nderkindo Perpetua Kessy, Dk. Twaha Issa Taslima, Abdullah Ali Hassan Mwinyi, Bernard Musomi Murunyana, Charles Makongoro Nyerere na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, anayeingia kwa wadhifa wake wa Uwaziri.

Wabunge wengine walioapishwa ni kutoka Kenya, Uganda, Rwanda 


Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, akila kiapo cha kulitumikia Bunge la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, jijini Arusha leo, wakati bunge hilo lilipoanza kikao chake cha kwanza jijini humo.

Mbunge Shy-Rose Banji akila kiapo wakati wa kikao hicho, jijini Arusha leo.

Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania katika Bunge la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, Alhaji Adam Kimbisa, akila kiapo.

 Anjela Charless Kizigha, akiapa kuwa Mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

Bernard Musomi Murunyana, akiapa kuwa Mbunge wa Bunge hilo.

Abdullah Ali Hassan Mwinyi, akila kiapo cha utiifu cha Bunge la Afrika ya Mashariki.
Nderkindo Perpetua Kessy, akila kiapo wakati wa kuwaapisha Wabunge wa Afrika ya Mashariki, jijini Arusha.

Charles Makongoro Nyerere, akiapa kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika ya Mashariki jijini Arusha leo.

Mbunge wa Afrika ya Mashariki, Dk. Twaha Issa Taslima, akiapa kulitumikia Bunge hilo, jijini Arusha leo wakati wa kikao cha kwanza cha Bunge hilo jijini humo. (Picha zote na Mroky Mroky)

No comments:

Post a Comment