Rais Salva Kiir amewaandikia wakuu wa serikali 75 wakiwemo mawaziri akiwataka warudishe jumla ya dola za marekani billioni 4 ambazo anadai walizopora kutoka hazina ya serikali yake.
Rais Kiir amesema serikali yake inahitaji pesa hizo sana kufuatia hatua ya kusimamisha uzalishaji wa mafuta kutoka kwa visima vyake baada ya mzozo na jirani yao Sudan.
Kupitia barua iliotumiwa viongozi hao yapata siku10 zilizopita, kiongozi huyo alielezea kuchukizwa kwake na hatua ya wakuu hao wa serikali ambao wametilia maanani mahitaji yao binafsi kuliko yale ya taifa hilo changa.
"Raia wa Sudan Kusini wanapata taabu lakini viongozi hawa wanafikiria tuu haja zao binafsi" alisema Rais Kiir kwenye barua hiyo.
Sudan Kusini ambayo ilijitenga na Sudan mwezi July mwaka jana inategemea sana mafuta ambayo yanachangia 98% ya kipato cha serikali hiyo changa.
Kenye barua hiyo, Rais Kiir amesema kuwa kiasi kikubwa cha pesa hizo kimewekwa kwenye benki za nchi za kigeni au zimetumika kununua majengo na mali nyengine katika nchi hizo.
Sudan Kusini imekuwa ikikabiliwa na tatizo kubwa la rushwa miongoni mwa wakuu wa serikali.
Msemaji wa serikali ambaye pia ni waziri wa habari Benjamin Marial Barnaba amesema zaidi ya dola bilioni 2 zilipotea katika kashfa moja inayohusisha mauzo ya zao la mtama.
No comments:
Post a Comment