Mwenyekiti wa Shina la Chama Cha Mapinduzi (CCM) la Pamba Road Posta Mpya, Said Masanga (wa pili kushoto), akisindikizwa na viongozi na wanachama wa CCM wa Kata ya Mzimuni Wilaya ya Kinondoni, wakati alipokuwa akirudisha fomu ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Wilaya ya Kinodnoni, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kada wa CCM, Amir Mwanahewa, Katibu Kata ya Mzimuni, Cheka Mgogo ( wa tatu) na Katibu wa Siasa na Uenezi wa Tawi la Lango la Jiji Magomeni, Suleiman Kitambi.
Mwenyekiti wa Shina la Chama Cha Mapinduzi (CCM) la Pamba Road Posta Mpya, Dar es Salaam, Said Masanga (mbele), akienda kurejesha fomu ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama hicho (UVCCM), Wilaya ya Kinondononi kwenye Ofisi za Umoja huo, wilayani humo leo.
Mwenyekiti wa Shina la Chama Cha Mapinduzi (CCM) la Pamba Road Posta Mpya, Dar es Salaam, Said Masanga akijaza maelezo kwenye kitabu kabla ya kukabidhi fomu zake za kugombea nafasi ya Uwenyekiti wa Umoja huo kwa Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja huo, wilayani humo, Abdallah Ngomandodo (kushoto), jijini leo.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mbezi Kati, Alhaj Salum Londa (kushoto), akisubiri kukabidhiwa fumo za kugombea nafasi za Ujumbe wa Mkutano Mkuu Taifa Vijana na Ujumbe wa Baraza Kuu la Vijana, Mkoa wa Dar es Salaam, kutoka kwa Msaidizi wa Katibu wa UVCCM, Kinondoni, Abdallah Ngomandodo (anayejaza fomu kulia), Ofisi za Umoja huo, Kinondoni jijini leo.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mbezi Kati, Alhaj Salum Londa (katikati), akiwa na baadhi ya viongozi na wanachama wa CCM, waliomsindikiza kuchukua fomu, wakimsubiri Msaidizi wa Katibu wa UVCCM, Kinondoni, Abdallah Ngomandodo (anayejaza fomu kulia), ili kumkabidhi fumo za kugombea nafasi za Ujumbe wa Mkutano Mkuu Taifa Vijana na Ujumbe wa Baraza Kuu la Vijana, Mkoa wa Dar es Salaam kwenye Ofisi za Umoja huo, Kinondoni jijini leo.
Katibu Kata wa Kawe, Aisha Katundu (kushoto), akimwelekeza jambo Mwenyekiti wa Mtaa wa Mbezi Kati, Alhaj Salum Londa, mara baada ya kukabidhiwa fomu za kugombea Ujumbe wa Mkutano Mkuu Taifa Vijana na Ujumbe wa Baraza Kuu la Vijana, Mkoa wa Dar es Salaam, wakati alipofika kwenye Ofisi za Umoja huo, Kinondoni jijini leo.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mbezi Kati, Alhaj Salum Londa, akijaza kitabu cha kuchulia fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wa Umoja wa Vijana Wilaya ya Kinodononi, mara baada ya kukabidhiwa fomu za kugombea nafasi za Ujumbe wa Mkutano Mkuu Taifa Vijana na Ujumbe wa Baraza Kuu la Vijana, Mkoa wa Dar es Salaam, Ofisi za Umoja huo, Kinondoni jijini leo.
No comments:
Post a Comment