TANGAZO


Friday, June 8, 2012

Rais Kikwete awaapisha Majaji na Makamishna wa Mahakama


Rais Jakaya Kikwete akimwapisha  Edward Rutakangwawa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama, katika hafla ya kuwaapisha Majaji wawili na Makamishna wa Mahakama, Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Wa pili kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue. 

Rais Jakaya Kikwete, akimwapisha Semistocles Kaijage, kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaani Tanzania, Ikulu Dar es Salaam leo. Kabla ya uteuzi huo, Semistocles Kaijage, alikuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, akifurahia jambo na Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama,  Edward Rutakangwa (wa pili kulia), mara baada ya kumwapisha Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Mussa Kipenka na Jaji  Semistocles Kaijage.

Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mussa Kipenka akipewa maua wakati alipokuwa akipongezwa na baadhi ya ndugu zake, waliohudhuria hafla hiyo fupi ya kuapishwa kwake kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete akimwapisha Edward Rutakangwa kuwa Kamishna  wa Tume ya Utumishi wa Mahakama katika hafla fupi iliyofanyika leo Ikulu jijini Dares Salaam.
Jaji wa Mahakama ya Rufaani, Semistocles Kaijage, akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kuapishwa  Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Pamoja na mambo mengine amesema atahakikisha kuwa anatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria, kupunguza mlundikano wa kesi na kuhakikisha kuwa maamuzi yanatolewa, yanatolewa kwa haki.

Jaji wa Mahakama ya Rufaani, Mussa Kipenka, akisaini hati ya kiapo mara baada ya kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Anayeshuhudia ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mohammed Chande Othman.

No comments:

Post a Comment