Mjomba wa marehemu Rozina Mwadala (60), aliyezikwa akiwa hai baada ya kutuhumiwa kujihusisha na imani za kishirikina katika Kijiji cha Malamba,Wilaya ya Mbarali,Mkoani Mbeya June 2,Bwana Wilson Legembo akiwa na mwandishi wa habari wa Kituo cha redio Baraka FM kilichopo jijini Mbeya Bwana Sifael George muda mfupi baada ya marehemu kuzikwa.Tukio hilo limekuja baada ya Mganga wa Jadi kutoka Wilaya ya Mbarali kupiga Ramli kwa madai kuwa marehemu aliyezikwa hai ndiye aliyesababisha kifo cha mkazi mwingine wa kijiji hicho marehemu Frank Lingo(25), aliyefariki Juni Mosi mwaka huu kwa maumivu kwenye sikio na jicho.
Viongozi wa Muungano wa Jamii Tanzania (MJATA) walifika eneo latukio siku moja baada ya tukio la mtu kuzikwa akiwa hai Bi. Rozina,kitendo ambacho walikilaana vikali na kuwataka Waganga wa jadi kutoleta uchonganishi unaopelekea watu wengi kuuwawa pasipo hatia.
Mchungaji wa Kanisa la Baptist Bwana John Laus (mzungu), hakusita kufika kwenye msiba kushuhudia tukio hilo la kikatili la mtu kuzikwa akiwa hai,ambapo aliwataka wananchi kutojichukulia sheria mkononi.
Viongozi wa MJATA wakiwa nyumbani kwa marehemu kutoa pole kwa wanafamilia na kukemea vitendo viovu,ambapo wameiomba Serikali kuchukua hatua za makusudi kwa wale wote waliohusika na tukio hili.
Baadhi ya akina mama waombolezaji wakiwa nje ya nyumba ya marehemu.
(Picha na Ezekiel Kamanga wa Mbeya Yetu Blog).
No comments:
Post a Comment