TANGAZO


Friday, June 8, 2012

BREAKING NEWS: Rais Kikwete ateu Majaji 10 wa Mahakama Kuu, yumo Msajili Mahakama ya Rufaa, Francis Mutungi

Mhe. Mutungi akizungumza jambo na Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti la Tanzania Daima, Happiness Katabazi.


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


Coat of Arms
PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI – UTEUZI WA MAJAJI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewateua Majaji 10 wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuanzia jana Alhamisi, Juni 7, 2012.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Y Sefue jioni ya leo, Ijumaa, Juni 8, 2012, walioteuliwa ni Ndugu Francis Sales Katabazi Mutungi, Ndugu Sam Mpaya Rumanyika, Ndugu Patricia Saleh Fikrini, Dkt. Gerald Alex Mbonimpa Ndika na Ndugu Salvatory Benedict Bongole.
Wengine walioteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania ni Ndugu Mathew Pauwa Mhina Mwaimu, Ndugu Jacob C.M. Mwambegele, Ndugu Latifa Mansoor, Ndugu John Samwel Mgetta na Ndugu Joaquine Antoinette De- Mello.
Kabla ya uteuzi wake Ndugu Mtungi alikuwa  Msajili wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Ndugu Rumanyika alikuwa Msajili wa Baraza la Rufani la Kodi, Ndugu Fikirini alikuwa Hakimu Mkazi Mkuu, Ndugu Ndika alikuwa Mkuu wa Chuo cha Sheria Tanzania na Ndugu Bongole alikuwa Naibu Msajili Mwandamizi, Mahakama Kuu.
Ndugu Mwaimu alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Haki za Binadamu, Ndugu Mwambegele alikuwa Msaidizi wa Katibu wa Baraza la Mawaziri, Ndugu Mansoor alikuwa Wakili katika Latifa Law Chambers, Ndugu Mgetta alikuwa Hakimu Mkazi Mkuu na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani na Ndugu De-Mello alikuwa Wakili wa Kujitegemea.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
8 Juni, 2012

1 comment:

  1. Am so happy on this news, i would like to send congrats to all but mostly to my good friend of mine Mhe: FRANCIS MUTUNGI. Mungu akutangulie katika kila jambo utakaloenda amua sasa. ongera sana, i have seen your future even before.

    ReplyDelete