TANGAZO


Thursday, June 7, 2012

Spika Makinda akutana na Mabalozi wa Sudan, Saudia na Jamhuri ya watu wa Saharawi

 Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda akimkaribisha Balozi wa Jamhuri ya Sudan, Dk. Yassir Mohamed Alli, wakati Balozi huyo, alipomtembelea Spika ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Balozi huyo alifika ofisini kwa Spika Makinda kwa ajili ya kuwasilisha barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Sudan, Ahmed Ibrahim Ali- Tahir, yenye ombi la Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Sudan kutaka kutembelea Tanzania kwa ziara ya mafunzo.

Spika wa Bunge, Anne Makinda akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Saudi Arabia, Hani Moninah, wakati Balozi huyo, alipomtembea Spika ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo. 

Spika wa Bunge, Anne Makinda akimuaga Balozi wa Jamhuri ya Watu  wa Saharawi, Brahim Salem Biget, wakati Balozi huyo, alipomtembelea ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo na kufanya nae mazungumzo. (Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge)

No comments:

Post a Comment