TANGAZO


Thursday, June 7, 2012

Nape afunika Makambako

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akihutubia umati wa watu kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana jioni, Juni 6, 2012, Uwanja wa Polisi, mji wa Makambako, Wilaya ya Njombe Mkoa mpya wa Njombe.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akizindua tawi la CCM, Ubena Makambako, akiwa katika ziara ya kuimarisha uhai wa Chama mkoani Njombe.


Mzee Leonard Mwampamba, akimkabidhi Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, mundu alipozungumza na wazee wa Ilembula, Wilaya ya Wanging'ombe, akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Njombe jana.


Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akisakata muziki na kijana wa Kata ya Ilembula, kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye Kata hiyo.


Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akizungumza na wazee wa Kata ya Ilembula, Wilaya ya Wanging'ombea, akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Njombe.


Nape akipuliza baragumu la kienyeji, alipokuwa akishiriki ngoma, wakati wa mapokezi yake Ilembula, Wilaya ya Wanging'ombea, akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Njombe.


Vijana wakionyesha umahiri wa kucheza sarakasi walipotumbuiza wakati wa mkutano wa CCM kwenye uwanja wa Polisi Makambako.


Nape akimsalimia mmoja wa wananchi, mwenye ulemavu, waliohudhuria katika mkutano wake wa Makambako.



Nape akishiriki kupiga ngoma pamoja na vijana wa Makambako, wakati alipofika hapo na kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara jana, akiwa katika ziara yake ya kuimarisha uhai wa Chama mkoani Njombe.

No comments:

Post a Comment