Spika wa Bunge, Anne Makinda, akifungua mafunzo maalum yaliyoandaliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kwa ajili ya kuwajengea uwezo Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa Kamati za Bunge katika kuchambua Bajeti ya Serikali, Bagamoyo mkoani Pwani leo.
Spika wa Bunge, Anne Makinda, akifungua mafunzo maalum yaliyoandaliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kwa ajili ya kuwajengea uwezo Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa Kamati za Bunge katika kuchambua Bajeti ya Serikali. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, John Cheyo na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali Ludovick Uttoh.
Baadhi ya Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa Kamati za Bunge wakiweka data zao kwenye kompyuta, wakati Spika Makinda, alipokuwa akitoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo maalum yaliyo andaliwa kwa ajili yao na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), katika kuwajengea uwezo wa kuchambua Bajeti ya Serikali, yaliyofanyika Bagamoyo leo.
Baadhi ya Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa Kamati za Bunge, wakifuatilia kwa makini hotuba ya ufunguzi kutoka kwa Spika Anna Makinda, wakati wa mafunzo maalum yaliyoandaliwa kwa ajili yao na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kuchambua Bajeti ya Serikali, yaliyofanyika Bagamoyo leo.
Mgeni Rasmi, Spika wa Bunge, Anne Makinda (katikati mbele waliokaa), akipiga picha ya kumbukumbu na Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa Kamati za Bunge wanaohudhuria mafunzo maalum yaliyo andaliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), wa kwanza kushoto, walikaa mbele, katika kuwajengea uwezo wa kuchambua Bajeti ya Serikali, yaliyofanyika Bagamoyo, mkoani Pwani leo. (Picha zote na Owen David)
No comments:
Post a Comment