TANGAZO


Saturday, June 2, 2012

Nape Nnauye aingarisha Miss Singida




Msanii Khadija Kopa akitumbuiza mashabiki wakati wa shindano la kumsaka mrembo wa  mjini Singida usiku wa kuamkia leo, ukumbi wa Aqua mjini Singida. 

 Katibu wa Kamati Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akienda  kumtuza fedha, msanii nguli wa miondoko ya tarab nchini, Khadija Kopa wakati alipokuwa akitumbuiza kwenye  shindano hilo.

Warembo walioingia tano bora, wakiwa wamepozi baada ya kuchaguliwa na majaji wa shindano hilo, usiku wa kuamkia leo, ukumbi wa Aqua mjini Singida. 

Miss Singida 2012, Zena Mondi (katikati),  akiwa na mshindi wa pili Rehema Marwa (kushoto) na mshindi wa tatu, Eliza Diamond, wakiwapungia mkono mashabiki waliofika kwenye shindano hilo, mara baada kutangazwa na kuvalishwa mataji yao, ukumbi wa Aqua mjini Singida. 

Miss Singida 2012, Zena Mondi (katikati),  akiwa na mshindi wa pili Rehema Marwa (kushoto) na mshindi wa tatu, Eliza Diamond, wakiwapungia  mashabiki, mara baada kutangazwa na kuvalishwa mataji yao, ukumbini hapo.


Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimkabidhi zawadi Miss Singida 2012, Zena Mode, mara baada ya kuibuka na kutangazwa mshindi, shindano la hilo
usiku wa kuamkia leo, Juni 2, 2012. Mshindi wa Kwanza amepata sh. 400,000, wapili sh. 300,000 na wa tatu sh. 200,000.  Wakati alipokuwa akifungua shindano hilo, Nape aliahidi  kwamba Chama cha CCM, kitatoa ajira kwa miss Singida kama atafanikiwa kuingia katika tatu bora katika shindano la Redd's Miss Tanzania 2012.


Nape akiwa na Miss Singida, Zena Mode (wa pili kushoto), mara baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi hao usiku wa kuamkia leo ukumbini hapo. Wengine ni mshindi wa Pili Rehema Marwa (kushoto) na  wa tatu, Eliza Diamond.


Wanyange wote wa kinyang'anyiro cha kumtafuta Redd's Miss Singida 2012, wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu wa Kamati Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye mara baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano hilo usiku wa kuamkia leo. (Picha zote na Bashir Nkoromo)


No comments:

Post a Comment