TANGAZO


Tuesday, June 19, 2012

Semina ya Wakufunzi wa Sensa yaendelea Dodoma

Baadhi ya wakufunzi wa Sensa kwa ngazi ya Kitaifa wakijifunza jinsi ya kutambua maeneo mbalimbali  ya sensa za watu na makazi kwa kutumia ramani jana mjini Dodoma, wakati wa  mafunzo  ya siku 10 kwa ajili ya kwenda kufundisha hatua za Mikoa ikiwa ni maandalizi ya Sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika nchini kote  Agosti 26, mwaka huu. Mafunzo hayo yanaendeshwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), yalianza  jana mjini Dodoma. 

Wakufunzi wa Sensa kwa ngazi ya Kitaifa wakisoma ramani kwa ajili ya kutambua maeneo mbalimbali ya kufanyia sensa pamoja na sehemu za mipaka ambayo kila karani atakuwa amepewa kufanyia zoezi hilo. Wakufunzi hao wako katika mafunzo  ya siku 10 kwa ajili ya kwenda kufundisha hatua za Mikoa ikiwa ni maandalizi ya Sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika nchini kote  Agosti 26, mwaka huu. Mafunzo hayo yanaendeshwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), yalianza  jana mjini Dodoma. 



Wakufunzi wa Sensa kwa ngazi ya Kitaifa wakielekezana jinsi ya kusoma ramani kwa ajili ya kutambua maeneo mbalimbali  ya sensa za watu na makazi wakati wa mafunzo  ya siku 10, mjini Dodoma jana kwa ajili ya kwenda kufundisha hatua za Mikoa ikiwa ni maandalizi ya Sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika nchini kote  Agosti 26, mwaka huu. Mafunzo hayo yanaendeshwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), yalianza  jana mjini Dodoma. (Picha zote na Tiganya vincent- Dodoma)



No comments:

Post a Comment