TANGAZO


Tuesday, June 19, 2012

Tume ya mabadiliko ya Katiba, yakutana na waandishi wa habari, Dar es Salaam

Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba, Jaji Mstaafu Joseph Warioba, akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam, jinsi tume hiyo ilivyokaribia kuanza kwa awamu ya kwanza ya mchakato wa kushauriana na wananchi katika ukusanyaji na kuratibu maoni ya Katiba mpya. Kulia ni Katibu wa Tume Asaa Rashid.


Baadhi ya wajumbe wa  Tume ya mabadiliko ya Katiba wakimsikiliza Jaji Mstaafu Joseph Warioba (hayupo pichani), wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu jinsi tume hiyo ilivyokaribia kuanza kwa awamu ya kwanza ya mchakato wa kushauriana na wananchi katika ukusanyaji na kuratibu maoni ya katiba mpya.


Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani), jinsi walivyo na nafasi  kubwa ya kufanikisha mchakato wa Katiba kwa kutangaza maoni ya wananchi ili waweze kuchagua aina ya Taifa na Katiba wanayoitaka. Wanaomsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya Katiba Jaji Mstaafu Joseph Warioba (katikati) na Katibu wa Tume Assaa Rashid.



Baadhi ya waandishi wa habari, wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko ya Katiba Jaji Mstaafu Joseph Warioba (hayupo pichani) akiwaelezea jinsi tume hiyo ilivyokaribia kuanza kwa awamu ya kwanza ya mchakato wa kuzunguka nchi nzima ili kushauriana na wananchi katika ukusanyaji na kuratibu maoni ya katiba mpya.


Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa Shirika la Habari la Uingereza Idhaa ya Kiswahili (BBC), Erick Nampesya akishukuru wa niaba ya wanahabari mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa mabadiliko ya katiba uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Mkutano huo uliandaliwa naTume ya mabadiliko ya katiba. 


Baadhi ya wajumbe wa  Tume ya mabadiliko ya Katiba, wakimsikiliza Jaji Mstaafu Joseph Warioba (hayupo pichani), wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu jinsi tume hiyo ilivyokaribia kuanza kwa awamu ya kwanza ya mchakato wa kushauriana na wananchi katika ukusanyaji na kuratibu maoni ya Katiba mpya, Dar es Salaam leo.



Mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko ya Katiba Jaji Mstaafu Joseph Warioba(kulia) akisalimiana na baadhi ya wajumbe wa tume hiyo mara baada ya kumaliza kuongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Tume hiyo karibu itaanza awamu ya kwanza ya mchakato wa kushauriana na wananchi katika ukusanyaji na kuratibu maoni ya katiba mpya. (Picha na Anna Nkinda - Maelezo)

No comments:

Post a Comment