TANGAZO


Monday, June 18, 2012

Rais Shein afungua semina ya Viongozi wa Kidini katika kukuza utalii, Zanzibar


Baadhi ya Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya Kidini wa Mkoa wa Mjini  Magharibi wakisikiliza  kwa makini hotuba ya ufunguzi wa  semina ya siku moja ya Viongozi wa Kidini
katika kukuza dhana ya Utalii kwa wote, iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja leo. (Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu)



Baadhi ya Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya kidini wakisikiliza  hotuba ya ufunguzi wa  semina ya siku moja ya Viongozi wa Kidini katika kukuza dhana ya Utalii kwa wote, iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, Mjini Unguja leo.



Baadhi ya Viongozi wa Madhehebu mbalimbali ya Kidini wa Mkoa wa Mjini  Magharibi wakisikiliza  hotuba ya ufunguzi wa  semina ya Viongozi wa Kidini katika kukuza dhana ya Utalii kwa wote, iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, Mjini Unguja leo.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akitoa hutuba yake katika ufunguzi wa semina ya siku moja kwa  Viongozi wa Kidini katika kukuza dhana ya Utalii kwa wote, iliyofanyika katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel, Mjini Unguja leo. Kulia ni Msahauri wa Rais masuala ya Utalii, Issa Ahmed Othman na Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo, Said Ali Mbarouk. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii, Ali Halil Mirza. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kidini katika kukuza dhana ya Utalii kwa wote, mara baada ya kuifungua semina hiyo ya siku moja, iliyofanyika katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja leo.

No comments:

Post a Comment