Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Amir Mhando, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kabla ya Mwenyekiti wa Chama hicho, Juma Pinto (katikati), kuzungumza kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya utoaji tuzo za wanamichezo bora na pia kumtaja Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi kuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, itakayofanyika kesho, ukumbi wa Diamond Jubilee jijini. Kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Serengeti Breweries (SBL), wadhamini wa tuzo hizo, Imani Lwinga. (Picha zote Kassim Mbarouk)
Baadhi ya waandishi wa habari, Dina Ismaili wa Mama Pipiro blogspot (kushoto) na Vicky Kimaro wa Gazeti la Mwananchi wakisikiliza habari zilizokuwa zikitolewa na viongozi wa Taswa kuhusu kukamilika kwa maandalizi hayo.
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Juma Pinto, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya utoaji tuzo za wanamichezo bora wa Chama hicho na pia kumtaja Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi kuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, itakayofanyika kesho, ukumbi wa Diamond Jubilee jijini. Kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Serengeti Breweries (SBL), wadhamini wa tuzo hizo, Imani Lwinga. (Picha zote Kassim Mbarouk)
Baadhi ya waandishi wa habari, kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakimsikiliza mwenyekiti wa Taswa, Juma Pinto, wakati alipokuwa akizungumza nao kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya utoaji tuzo hizo na pia alipomtangaza Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi kuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, itakayofanyika kesho, ukumbi wa Diamond Jubilee jijini.
Baadhi ya waandishi wa habari, kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia habari hizo zilizokuwa zikitolewa na Mwenyekiti wa Taswa, Juma Pinto, wakati alipokuwa akizungumza nao kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya utoaji tuzo hizo na pia alipomtangaza Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi kuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, itakayofanyika Diamond Jubilee jijini kesho.
Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pint, akijibu maswali ya waandishi wa habari katika hafla hiyo. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Taswa, Maulid Kitenge na katikati ni Katibu Mkuu wake, Amir Mhando.
No comments:
Post a Comment