TANGAZO


Tuesday, June 12, 2012

Hodgson asema England itakuwa imara

England na Ufaransa
Roy Hodgson anasema ana imani timu yake ya England itaimarisha kiwango cha mchezo kadri inavyocheza mechi zaidi
Kocha wa timu ya taifa ya soka ya England, Roy Hodgson, amesema sare ya 1-1 dhidi ya timu ya Ufaransa, ambayo inasemekana ndio timu bora zaidi katika kundi lao, ni dalili kwamba vijana wake wanaweza kuinua kiwango cha mchezo wao katika michuano ya Euro 2012.
Timu zote Jumatatu ziliweza kuonyesha mbinu nzuri na kila upande kwa muda kuweza kumiliki mpira kwa muda katika uwanja wa Donetsk, huku jua kali likiangaza, na Joleon Lescott akipata bao la kwanza la England, kabla Samir Nasri kusawazisha.
"Hii ni nafasi nzuri kwetu kuweza kuimarisha mchezo wetu,” alisema Hodgson baada ya mechi yao ya kwanza, katika kundi D.
"Ni matumaini yetu kwamba tutakuwa bora zaidi. Kadri tunavyofanya mazoezi na kucheza mechi nyingi, ndivyo tunavyoimarisha mchezo wetu zaidi.”
Hii ilikuwa ni mechi ya tatu kwa Hodgson tangu achukue hatamu za kuiongoza timu ya taifa ya soka ya England.
Alielezea kwamba aliridhika na mchezo huo, baada ya kutoka sare na timu ya Ufaransa, ambayo haijashindwa katika kipindi cha miaka miwili.
Katika mechi ya pili siku ya Jumatatu, Ukraine iliweza kuishinda Sweden magoli 2-1

No comments:

Post a Comment