TANGAZO


Sunday, June 3, 2012

Rais Kiwete, afanya mazoezi ya kujijenga kiafya

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, aliye katika mapumziko mafupi jijini Arusha, akiwa katika mazoezi yake ya  kutembea kilomita tatu kila asubuhi na jioni kabla ya  kufanya mazoezi ya viungo na kuingia gym, katika kuuweka mwili wake katika hali ya ukakamavu na afya. Wakaazi wengi wa jijini Arusha ambao wamemuona Rais Kikwete akitembea wakati wa mazoezi hayo, wamesisimkwa na kufurahishwa sana na hatua hiyo ya Kiongozi Mkuu wa Nchi kuwa mstari wa mbele katika kujenga afya kwa mazoezi ya kila siku na kutaka kila mtu, awe anafanya mazoezi hayo na si viongozi tu, ili kuiga mfano wake. (Picha na Ikulu)


Rais Jakaya Mrisho Kikwete,  akitembea wakati wa mazoezi hayo ya kilomita tatu, asubuhi na jioni kabla ya  kufanya mazoezi ya viungo kwenye gym kwa ajili ya kuuweka mwili wake katika hali ya ukakamavu na afya. 


Rais Jakaya Mrisho Kikwete, alikinyoosha na kukunja misuli yake katika kujiweka sawa na mazoezi ya gym hapo baadaye. 


Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akitoka kwenye mazoezi ya kutembea kilomita tatu asubuhi ya leo na kisha kurudia tena jioni kabla ya  kufanya mazoezi ya viungo na kuingia gym, katika kuuweka mwili wake katika hali ya ukakamavu na afya. 

No comments:

Post a Comment