Patricia Fikirini, akiapa mbele ya Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani), kuwa Jaji wa Mahakama Kuu, wakati Rais alipokuwa akiwaapisha Majaji 10, viwanja vya Ikulu jijini, aliowateu Juni 7, mwaka huu.
Jaji Sam Rumanyika, akiapa mbele ya Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani), kuwa mwaminifu katika kazi yake ya Ujaji wa Mahakama Kuu aliyoteuliwa, kwa Rais na kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati wa hafla ya kuwaapisha majaji 10, aliowateua hivi karibuni.
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Francis Mutungi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha majaji 10, iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Rais Kikwete aliowateua Majaji hao Juni 7, mwaka huu.
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha John Mgetta kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha majaji 10, iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Rais Kikwete aliowateua Majaji hao Juni 7, mwaka huu.
Rais Jakaya Kikwete, akiweka saini hati ya kiapo cha Latifa Mansoor, mara baada ya kuapa kwa nafasi ya Jaji wa Mahakama Kuu, aliyoteuliwa na Rais hivi karibuni, wakati wa hafla ya kuwaapisha majaji 10 wapya wa Mahakama Kuu, Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Naibu waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki (kushoto), akiwa na Jaji Mkuu, Mohamed Othman Chande (kulia), Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema ( wa pili kulia) na Jaji Kiongozi Faki Jundu.
Rais Jakaya Kikwete, akielekea kwenye viwanja vya kupigia picha za kumbukumbu, akifuatana na Jaji Mkuu Mohamed Othman Chande (kulia), huku wakibadilishana mawazo.
Rais Jakaya Kikwete, akipiga picha ya kumbukumbu na Maji wapya 10, baada ya kuwaapisha Ikulu Dar es Salaam leo. Kulia kwa Rais ni Jaji Mkuu, Mohamed Othman Chande na kushoto ni Jaji Kiongozi Faki Jundu.
Rais Jakaya Kikwete, akipiga picha ya kumbukumbu na Jaji Francis Mutungi na familia yake mara baada ya kuwaapisha majaji 10 wapya wa Mahakama Kuu, Ikulu Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete, akipiga picha ya kumbukumbu na Jaji Salvatory Bongole pamoja Maofisa mbalimbali wa Ikulu mara baada ya kuwaapisha majaji 10 wa Mahakama Kuu, Ikulu Dar es Salaam leo.Rais Jakaya Kikwete, akipiga picha ya kumbukumbu na Jaji Latifa Mansoor pamoja na familia yake mara baada ya kumuapisha katika hafla ya kuwaapisha majaji 10 wa Mahakama Kuu, Ikulu Dar es Salaam leo.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kushoto), akizungumza na Jaji Mkuu, Mohamed Othman Chande wakati Rais Jakaya Kikwete, alipowaapisha majaji wa Mahakama Kuu 10, viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam leo. Kulia ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema.
Rais Jakaya Kikwete, akizunguma jambo na Jaji Mkuu, Mohamed Othman Chande (kulia), Rais, alipokuwa katika hafla ya kuwaapisha majaji 10 wapya wa Mahakama Kuu, Ikulu Dar es Salaam leo.
Jaji Francis Mutungi akizungumza jambo na familia yake mara baada ya kuapishwa na Rais Kikwete, wakati wa hafla ya kuwaapisha majaji 10 wapya wa Mahakama Kuu, Ikulu Dar es Salaam leo.
Jaji Mkuu, Mohamed Othman Chande, akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam leo, mara baada ya Rais Jakaya Kikwete, kuwaapisha majaji 10 wapya wa Mahakama Kuu.
Rais Jakaya Kikwete, akizungumza na baadhi ya wageni waliokuwepo katika hafla ya kuwaapisha majaji wapya 10 wa Mahakama Kuu, Ikulu Dar es Salaam leo. Kushoto ni Jaji Kiongozi Faki Jundu.
Rais Jakaya Kikwete, akipiga picha ya kumbukumbu na Jaji John Mgetta pamoja na familia yake mara baada ya kuwaapisha majaji 10 wa Mahakama Kuu, Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
No comments:
Post a Comment