TANGAZO


Tuesday, June 19, 2012

Rais Kikwete akutana na uongozi Shirikisho la Mpira Kikapu

Rais Jakaya Kikwete akisikiliza maelezo kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Mussa Mziya wakati viongozi wa Shirikisho hilo walipomtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam leo ambapo walimueleza mipango mbalimbali waliyokusudia kuitekeleza, ikiwemo timu ya Taifa ya mchezo huo, kushiriki katika mashindao ya Afrika pamoja na kuandaa fainali za michuano hiyo nchini. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Phares Magessa (kulia), akimpatia maelezo Rais Kikwete, kuhusu mipango waliyokusudia kuitekeleza katika kuukuza mchezo huo nchini, walipomtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam leo, kumkabidhi jezi na vifaa vingine vya mchezo huo kutoka timu ya Ligi Kuu ya NBA ya New York Nicks ya Marekani, vilivyoletwa nchini na Mkufunzi Greg Brittenham kutoka timu hiyo, alipokuja nchini kutoa mafunzo kwa vijana hivi karibuni. 

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania, Mussa Mziya (kushoto) na Makamu wake, Phares Magesa (kulia), wakimkabidhi Rais Jakaya Kikwete jezi yenye jina lake, aliyopewa zawadi na timu ya Ligi Kuu ya NBA ya New York Nicks ya Marekani, iliyoletwa nchini na Mkufunzi Greg Brittenham kutoka timu hiyo, alipokuja nchini kutoa mafunzo kwa vijana hivi karibuni. 



Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania, Mussa Mziya (kushoto) na Makamu wake, Phares Magesa (kulia), wakimkabidhi Rais Jakaya Kikwete suti ya michezo, aliyopewa zawadi na timu ya Ligi Kuu ya NBA ya New York Nicks ya Marekani, iliyoletwa nchini na Mkufunzi Greg Brittenham kutoka timu hiyo, alipokuja nchini kutoa mafunzo kwa vijana hivi karibuni. 


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania, Mussa Mziya (kushoto) na Makamu wake, Phares Magesa (kulia), wakimkabidhi Rais Jakaya Kikwete mpira wa mchezo huo, aliyopewa zawadi na timu ya Ligi Kuu ya NBA ya New York Nicks ya Marekani, ulioletwa nchini na Mkufunzi Greg Brittenham kutoka timu hiyo, alipokuja nchini kutoa mafunzo kwa vijana hivi karibuni. 


 Rais Jakaya Kikwete, akipiga picha ya kumbukumbu na Uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), wakati ulipomtembelea kwa ajili ya kumkabidhi zawadi za vifaa vya mchezo huo kutoka timu ya Ligi Kuu ya NBA ya New York Nicks ya Marekani, vilivyoletwa nchini na Mkufunzi Greg Brittenham kutoka timu hiyo, alipokuja nchini kutoa mafunzo kwa vijana hivi karibuni. 


 Rais Jakaya Kikwete, akiagana na Marry Mmbaga, Mhazini wa TBF, wakati uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), ulipomtembelea kwa ajili ya kumkabidhi zawadi za vifaa vya mchezo huo kutoka timu ya Ligi Kuu ya NBA ya New York Nicks ya Marekani, vilivyoletwa nchini na Mkufunzi Greg Brittenham kutoka timu hiyo, alipokuja nchini kutoa mafunzo kwa vijana hivi karibuni. 


Rais Jakaya Kikwete, akiagana na Uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), wakati ulipomtembelea kwa ajili ya kumkabidhi zawadi za vifaa vya mchezo huo kutoka timu ya Ligi Kuu ya NBA ya New York Nicks ya Marekani, vilivyoletwa nchini na Mkufunzi Greg Brittenham kutoka timu hiyo, alipokuja nchini kutoa mafunzo kwa vijana hivi karibuni. 

No comments:

Post a Comment