Katibu Tawala mpya wa Mkoa wa Ruvuma, Hassan Mpapi Bendeyeko, akila kiapo mbele ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI), Dk. Aldin Mutembei, akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete kitabu cha kwanza cha fasihi simulizi za jamii ya Wakwere, Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Kulia anayeshuhudia ni Mkuu wa Idara ya Historia katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Kapepwa Tambila. Dk. Mutembei ambaye pia ni mchapishaji na msimamizi wa tafiti za Tamaduni, Lugha na Fasihi za makabila ya Tanzania, alikabidhi pia kamusi asisi ya Kiingereza - Kiswahili na Kiarabu. (Picha na Freddy Maro).
No comments:
Post a Comment