TANGAZO


Wednesday, June 20, 2012

Rais Kikwete akutana na Viongozi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Sirika la Nyumba Dodma


Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika mkutano na viongozi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Ikulu mjini Dodoma leo. Katika kikao hicho, Rais Kikwete aliwapa changamoto viongozi hao ya  kuunganisha nguvu na kubuni mikakati itakayowezesha kuwapatia watumishi wa umma nyumba za kuishi.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akisisitiza jambo wakati akiongea na Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Eriyo, mjini Dodoma leo, baada ya kikao maalumu na viongozi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dodoma leo..

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), mara baada ya kikao maalumu kilichofanyika Ikulu mjini Dodoma leo. Viongozi wengine waandamizi waliohudhuria kikao hicho, ni Naibu Waziri wa Ardhi Goodluck Ole Medeye (watatu kushoto),Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (Wanne kushoto),Gavana wa Benki Kuu Professa Beno Ndulu (kulia) na Naibu Katibu Mkuu Hazina Dk.Servacius Likwelile. Katika kikao hicho, Rais aliwapa changamoto viongozi hao ya kuunganisha nguvu na kubuni mikakati itakayowezesha kuwapatia watumishi wa umma nyumba za kuishi.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemiah Mchechu mara baada ya kikao maalumu kilichofanyika Ikulu mjini Dodoma leo

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau, akiteta jambo na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu, mjini Dodoma leo. (Picha zote na Freddy Maro)


No comments:

Post a Comment