TANGAZO


Wednesday, June 20, 2012

Bye Bye Kamanda wetu Willy Edward, unaenda lakini tutakukumbuka siku zote


Baadhi ya Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari nchini, wakilishusha jenenza lililokuwa na mwili wa marehemu, Willy Edward katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kufanyiwa Ibada na kuagwa na kisha kusafirishwa kwenda nyumbani kwao mjini Mugumu, mkoani mara kwa mazishi.

Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, akiteta jambo na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, wakati wa hafla ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Willy Edward, Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam leo.

Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi akipeana mkono huku wakifurahi na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi (CCM), Nape Nnauye na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, wakati wa hafla hiyo, walipokuwa wakibadilishana mawazo.

Baadhi ya waombolezaji akiwa katika hafla hiyo, viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam leo mchana.

Baadhi ya waandishi wa habari waandamizi wa vyombo mbalimbali wakiwa kwenye viwanja hivyo wakati wa Ibada ya kuaga mwili wa Willy Edward.

Mkuu wa Masoka na Mawasiliano wa benki ya NMB, Imani Kajula (kushoto), akimfaraji Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda, wakati wa Ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo leo, marehemu Willy Edward.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda, akisom wasifu wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, marehemu, Willy Edward wakati wa Ibada ya kuga mwili wake viwanja vya Mnazi Mmoja jijini leo.
Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi akizungumza kwa niaba ya wamiliki wa vyombo vya habari, kala ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, marehemu Willy Edward leo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts inayomilikitoa Gazeti la Jambo Leo na jarida la Jambo Brand, Juma Pinto, akizungumza wakati wa hafla ya kuuaga mwili wa aliyekuwa mhariri mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward, aliyefariki ghafla Jumamosi usiku, mjini Morogoro, ambapo maiti yake imesafirishwa kwa ajili ya mazishi mjini Mugumu, Mara.

  Waandishi, na wafanyakazi wa gazeti la Jambo Leo, wakiuaga mwili wa Willy Edward wakati wa hafla hiyo.

Mke wa marehemu Willy Edward, Rehema (kushoto), mdogo wake, Essy Ogunde na watoto, Kaleb (aliyepakatwa) na Colman (anayefutwa machozi), wakiwa katika hafla ya kuuaga mwili huo.

Mwenyekiti wa Makampuni ya tsn, Farough Baghozah (kushoto), Mkurugenzi wa Jambo Leo, Benny Kisaka, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya timu ya Yanga, Ridhwan Kikwete na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Felix Mosha, wakiwa katika hafla ya kuuaga mwili huo.

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba (kushoto), Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye (katikati) na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, wakiteta jambo wakati wa kuaga mwili wa marehemu Willy Edward.

 Baadhi ya wafanyakazi na waandishi wa gazeti la Jambo Leo, wakiwa katika hafla ya kuuaga mwili huo.

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, akitoa salama za rambirambi kwa niaba ya vyama vya upinzani wakati wa hafla hiyo.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi (CCM), Nape Nnauye akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Chama chake.

Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi akitoa heshima za mwisho.



Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi akimpa pole mjane wa marehemu, Rehemaheri Willy.

Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi (katikati), akimpa pole kaka wa marehemu Willy Edward, Denis Ongiri wakati wa kuuaga mwili huo leo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts, Juma Pinto.

Mhariri wa picha wa gazeti la Habario Leo na Daily News, Athuman Hamisi akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Willy Edward.

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, akitoa hesima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu Willy Edward.

Wahariri wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa marehemu Willy Edward.
Mkuu wa Uhasibu na Utawala cha gazeti la Jambo Leo, Vicky Muhere (akisaidiwa na mfanyakazi wa Kampuni ya Business Times, Sofia Mshangama, baada ya kushindwa kujizuia wakati akiaga mwili huo.

Baadhi ya wahariri na waandishi waandamizi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari wakitoa heshima za misho kwa mwili wa marehemu Willy Edward.
Wasanii wa bendi ya Twanga Pepeta, wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa mhariri mkuu wa gazeti la Jambo Leo, marehemu Willy Edward, ambaye alikuwa mmoja wa wapenzi wakubwa wa bendi hiyo.
Mtoto wa marehemu, Collman Willy akitoa heshima za mwisho.
Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari, wakilibeba jenenza lililowekwa mwili wa marehemu Willy Edward kwa ajili ya kwenda kuingwizwa kwenye gari tayari kwa safari ya kuelekea mjini Mugumu, Serengeti mkoani Mara.


Mhariri Mkuu wa gazeti la Tanzania Daima, akiwa ameibeba picha ya marehemu Willya wakati wa kutolewa jenenza lake kueleka kwenye gari tayari kwa safari ya Mugumu, mkoani Mara kwa mazishi.

No comments:

Post a Comment