TANGAZO


Tuesday, June 5, 2012

Onesho la Sugu Dar live usipime, mashabiki wapagawa


Msanii wa miondoko ya Hip Hop na  Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Mbilinyi 'Mr II' a.k.a Sugu, akiimba wakati alipokuwa akitumbuiza mashabiki wake waliofurika ndani ya ukumbi wa Dar Live, Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam juzi, wakati wa onesho lake la makamuzi lililojulikana kwa jina la  Usiku wa Sugu. Katika onesho hilo, Sugu alisindikizwa na wasanii Juma Nature, Profesa Jay, Vinega, Mkoloni na wengine wengi. Anayeimba naye ni Msanii Fredy Mariki 'Mkoloni'.

Mbunge wa Arumeru Mashariki kupitia Chadema, Joshua Nassari,  akitoa 'verse' mbele ya msanii Sugu, Mr II (nyuma), wakati wa onesho hilo la Usiku wa Sugu ndani ya Dar Live.

Profesa Jay akiwapagawisha mashabiki wakati akitoa burudani kwenye onesho hilo, ukumbi wa  Dar Live, Mbagala Zakhem usiku wa kuamkia leo.

Juma Nature na kundi lake la Wanaume Halisi likifanya makamuzi stejini katika onesho la Usiku wa Sugu.

msanii Suma G, alikifanya vitu vyake ukumbini hapo katika onesho la Usiku wa Sugu, Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.

Mbunge wa Jimbo la Kinondoni kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Idd Azzan akiwasalimia mashabiki wake, kwenye onesho hilo, ukumbi wa Dar Live jijini Dar es Salaam.

Umati wa mashabiki ukiwa umepagawa, wakati wasanii hao walipokuwa wakitumbuiza ukumbini hapo. 

Baadhi ya mashabiki wakipiga picha na msanii Sugu kwa ajili ya kupata kumbukumbu ya onesho hilo. (Picha zote na mpigapicha wetu)

No comments:

Post a Comment