TANGAZO


Monday, June 4, 2012

Washindi 5 wa Redd's Miss Kurasini watembelea Ofisi za Jambo Leo

Kaimu Mhariri Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Julian Msacky, akizungumza na washindi 5 wa shindano la Redd's Miss Kurasini 2012, wakati walipotembelea Ofisi za gazeti hilo, zilizopo makutano ya Mitaa ya Samora na Azikiwe, Dar es Salaam leo. Wa pili kushoto ni Mwandishi Mwandamizi wa Michezo wa Jambo Leo, Asha Kigundula.
Mwandishi wa habari mwandamizi wa Gazeti la Jambo Leo, Ebeniezer Mende, akiwakaribisha  washindi 5 wa shindano la Redd's Miss Kurasini 2012, wakati walipotembelea Ofisi za gazeti hilo, zilizopo makutano ya Mitaa ya Samora na Azikiwe, Dar es Salaam leo.
Mhariri wa Gazeti la Jambo Leo Jumapili, Said Mwishehe, akizungumza na washindi 5 wa shindano la Redd's Miss Kurasini 2012, wakati walipotembelea Ofisi za gazeti la Jambo Leo, zilizopo, makutano ya Mitaa ya Samora na Azikiwe, Dar es Salaam leo.
Mmoja wa wapigapicha wa Gazeti la Jambo Leo, Dotto Mwaibale, akiwaonesha jinsi picha za habari zinavyohifadhiwa na kisha kutumika kwenye gazeti, washindi 5 wa shindano la Redd's Miss Kurasini 2012, wakati walipotembelea Ofisi za gazeti hilo, zilizopo makutano ya Mitaa ya Samora na Azikiwe, Dar es Salaam leo.

Msanifu kurasa wa jarida la Jambo Brand, Elizabeth Mkeleja, akiwaeleza jinsi kurasa za gazeti hilo anavyozitengeneza kabla ya kuprintiwa na kuwa jarida kamili washindi 5 wa shindano la Redd's Miss Kurasini 2012, wakati walipotembelea Ofisi za gazeti la Jambo Leo, ambalo pia hutoa jarida la Jambo Brand, makutano ya Mitaa ya Samora na Azikiwe, Dar es Salaam leo. Kulia  ni Mwandishi Mwandamizi wa Michezo wa Jambo Leo, Asha Kigundula.
Msanifu kurasa wa jarida la Jambo Brand, Elizabeth Mkeleja, akiwafahamisha washindi 5 wa shindano la Redd's Miss Kurasini 2012, jinsi anavyozitengeneza kurasa la jarida hilo, wakati walipotembelea Ofisi za gazeti la Jambo Leo, ambayo pia jarida hilo, makutano ya Mitaa ya Samora na Azikiwe, Dar es Salaam leo. Wa pili kushoto ni Mwandishi Mwandamizi wa Michezo wa Jambo Leo, Asha Kigundula.
Msanifu kurasa wa Gazeti la Jambo Leo, Hamza Ally, akiwaonesha washindi 5 wa shindano la Redd's Miss Kurasini 2012, jinsi anvyozitengeneza kurasa la gazeti hilo, wakati walipotembelea Ofisi za gazeti hilo, makutano ya Mitaa ya Samora na Azikiwe, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwandishi Mwandamizi wa Michezo wa Jambo Leo, Asha Kigundula.
Msanifu kurasa wa Gazeti la Jambo Leo, Hamza Ally (wa tatu kulia), akipiga picha ya kumbukumbu pamoja na washindi 5 wa shindano la Redd's Miss Kurasini 2012, wakati walipotembelea Ofisi za gazeti hilo, makutano ya Mitaa ya Samora na Azikiwe, Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment