Mtayarishaji Mwandamizi wa
Vipindi vya Televisheni wa Shirika la
la Utangazaji Tanzania (TBC), Jeff
Shellembi (kulia), akimuonesha Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Amos Makalla (kushoto),
kaseti za kurekodi habari na vipindi mbalimbali. Alimueleza kwamba kanda yenye rangi
yekundu na bluu ni iliyochini ya
kiwango ambayo hudumu kwa miezi mitatu na kuathiri utendaji kazi, wakati alipofanya ziara leo kwenye kituo hicho cha televisheni
cha TBC, Mikocheni jijini Dares Salaam. Wa pili kushoto ni Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Joe Rugarabamu na
aliyevaa kitenge ni Mkurugenzi wa Habari na Matukio wa TBC, Suzan Mungy.
Fundi Mitambo wa Shirika la Utangazaji
Tanzania (TBC), Ally Kagomba akimuonesha Naibu Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla mitambo ya kurushia vipindi mbalimbali wakati wa Naibu Waziri huyo, alipofanya ziara kwenye kituo
cha televisheni cha TBC, leo Mikocheni jijini Dares Salaam.
Waziri Naibu Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Amos Makalla (katikati), akizungumza na wajumbe wa Bodi na uongozi wa Shirika la Utangazaji Tanzania ( TBC), mara baada
kumaliza ziara yake katika shirika hilo.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Amos Makalla (katikati), akiagana na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Utangazaji Tanzania( TBC), Wilfred
Nyachia baada ya kumaliza ziara
yake katika shirika hilo leo. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Joe Rugarabamu. (Picha zote na Magreth Kinabo-Maelezo)
No comments:
Post a Comment