TANGAZO


Friday, June 1, 2012

Chipukizi wapewa shavu kwa Dogo Aslay

Dodo Aslay, akiwa kazini huku akiwa amezungukwa na mashabiki wake kwenye moja ya maonesho ya kundi lake, jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu
Kampuni ya Ruhazi Promotion ya jijini Dar es Salaam, imewapa shavu wasanii kumi chipukizi kutoka Mkoani Dodoma kuonyesha vipaji vyao kabla ya onyesho la kumtambulisha chipukizi anayetamba hivi sasa katika Bongo Fleva, Asilahi Isihaka ‘Dogo Aslay’ katika maonyesho yajulikanayo kama Dodgo Aslay Live.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu jana, mratibu wa onyesho la Dodoma litakalofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri Juni 9, 2012 Jackline Masano alisema kuwa wameamua kutoa nafasi hiyo adimu kwa vijana wanaoibukia ili kuibua vipaji zaidi vya wasanii chipukizi wa mkoani Dodoma.
Jackline alisema kuwa wanaamini wanalo jukumu la kuwasaidia vijana hao kujitangaza kwa kuwa wengi wao wanatoka katika familia masikini hivyo kukosa fedha za kuingia studio kurekodi nyimbo, huku pia wakikwepwa na waratibu wengi pindi wanapoomba kutumbuiza kwenye maonyesho mbali mbali.
“Katika onyesho letu la Dogo Aslay Live litakalofanyika Uwanja wa Jamhuri Dodoma hapo Juni 9, 2012, tumetoa nafasi kumi kwa wasanii chipukizi wa mkaoni Dodoma kutumbuiza, tumefanya hivi ili kuwasaidia kuonnyesha vipaji vyao na kuwapa uzoefu wa kutumbuiza mbele ya mashabiki wengi na  kiingilio chetu pale Jamhuri ni sh 3000 kwa kila mtu,” alisema Jackline.
Alisema katika onyesho hilo wasanii mbali mbali maarufu nchini watatumbuiza akiwemo Abbas Hamisi ‘20%’, Mfalme wa Rhymes nchini Selemani Msindi ‘Afande Sele’ wa Morogoro, kundi la TMK Wanaume Family na Kituo cha kuibua vipaji cha Mkubwa na Wanawe cha jijini Dar es Salaam , ambacho kilimuibua Dogo Aslay.
Jackline alisema mbali ya onyesho hilo litakalofanyika mchana kwenye uwanja wa Jamhuri, siku hiyo usiku kutakuwa na shoo maalum kwa wale waliokosa nafasi mchana ambapo burudani kutoka kwa wasanii hao wote itahamia kwenye ukumbi wa Royal Village mjini humo.
Aidha Kampuni ya Ruhazi Promotion ya Dar es Salaam, imebainisha kuwa baada ya maonyesho hayo mawili kwa mpigo ndani ya Dodoma burudani itahamia jijini Arusha ambapo Jumamosi Juni 16, 2012  wasanii hao wote na wengine watakaotangazwa baadaye watafanya vituo vyao kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.

No comments:

Post a Comment