Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah, akizungumza wakati wa kukabidhi bendera kwa timu ya Taifa Stars, Dar es Salaam leo. (Picha na Kassim Mbarouk)
Kocha wa timu ya Taifa Stars, Kim Poulsen, akizungumza Meneja wa timu hiyo, Leopold Tasso, wakati wa kukabidhiwa bendera timu hiyo ya Taifa kwa ajili ya kwenda kucheza mchezo wa marudio na timu ya Taifa ya Msumbiji kuwania nafasi ya kushiriki Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Afrika Kusini.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodger Tenga, akizungumza wakati wa kukabidhi bendera kwa timu ya Taifa Stars, Dar es Salaam leo kwa ajili ya safari yao ya Msumbiji kurudiana na timu ya taifa ya nchi hiyo katika kuwania tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Afrika Kusini.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Taifa Stars wakiwa katika hafla hiyo, jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Taifa Stars, wakiwa katika hafla hiyo, wakimsikiliza mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Macky Sadik, jijini Dar es Salaam leo.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Macky Sadik, akizungumza katika hafla hiyo ya kukabidhi bendera kwa timu ya Taifa Stars, jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Taifa Stars, wakimsikiliza mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik.
Kocha wa timu ya Taifa, Kim Poulsen, akizungumza katika hafla hiyo, mara baada ya Mkuu wa Mkoa kukabidhi bendera.
Kapetani wa timu ya Taifa Stars, Juma Kaseja, akizungumza katika hafla hiyo, ambayo aliahidi kujituma kwa wachezaji wake ili kuliletea Taifa ushindi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik, akisalimiana na Meneja wa timu ya Taifa, Leopold Tasso Mukebezi wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik, akisalimiana na mchezaji Shomari Kapombe wa Taifa Stars katika hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik, akisalimiana na wachezaji wa Timu ya Taifa Stars.
Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Taifa Stars, Mwinyi Kazimoto (kushoto), Juma Nyosso (katikati) na Mbawana Samatta.
No comments:
Post a Comment