TANGAZO


Thursday, June 14, 2012

Simu ya Samsun inayoweza kufukuza mbu yaingia, yazinduliwa nchini


 Meneja wa Samsung Electronics Tanzania, Kishor Kumar (kushoto) akionesha simu aina ya Samsung Galaxy Pocket Smartphone ya bei nafuu inayouzwa sh. 199,000, ambayo pamoja na kuwa na vitu vingi vilevile ina uwezo wa kufukuza mbu.

Meneja wa Rejareja wa Kampuni hiyo, Sylvester Manyala (kulia), akimpatia simu mwandishi wa habari wa Gazeti la Tanzania Daima, Amana Nyembo, aliyeshinda bahati nasibu wakati wa uzinduzi wa simu hiyo, Dar es Salaam leo.
 Mwandishi wa habari wa kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Peter Shadrack (kushoto) akipokea zawadi ya simu kwa niaba  ya mwandishi mwenzie wa Channel Ten Fred Mwanjala aliyeshinda bahati nasibu hiyo, wakati wa uzinduzi wa simu hiyo jijini leo.

 Mwanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Dar es Salaam, Belinda Lanuo, akielezea jinsi anavyonufaika na simu hiyo, yenye mambo mbalimbali.
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kampala cha  jijini Dar es Salaam (KIU), akielezea mbele ya waandishi wa habari, jinsi simu hiyo, inavyomsaidia katika masuala yake ya elimu.

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Uandishi wa Habari (SJMC), Grace Kijo akionesha kwenye simu hiyo sehemu ambayo ukiweka inaweza kufukuza mbu. (Picha zote na Richard Mwaikenda)

No comments:

Post a Comment