TANGAZO


Sunday, June 3, 2012

Mkutano wa uzinduzi wa Kitabu cha maoni ya Waislamu kuhusu Katiba mpya

Umati wa Waislamu ukiwa ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam leo, wakati wa mkutano wao wa uzinduzi wa Kitabu cha Maoni ya Waislamu kuhsu Katiba mpya na kujadili masuala mbalimbali yaliyojitokeza nchini hivi karibuni. (Picha zote na Dotto Mwaibale)


 Mmoja wa Masheikh waliokuwa wakizungumza kwenye mkutano huo, akizungumza na umati uliojitokeza kuhusu matatizo yaliyojitokeza kwenye Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), yanayohusu  kubadilishwa kwa mtihadi wa Somo la Maarifa ya Uislamu.


Umati wa Waislamu ukiitikia Takbir wakati wa mkutano huo, ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam leo, kwenye uzinduzi wa Kitabu cha Maoni ya Waislamu kuhsu mchakato wa Katiba mpya na kujadili masuala mbalimbali yaliyojitokeza nchini hivi karibuni.


Baadhi ya Viongozi wa Dini ya Kiislamu waliokutana na Waislamu, ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam leo, kwa ajili ya kuzindua Kitabu cha Maoni yao kuhusu mchakato wa Katiba Mpya na kujadili masuala mbalimbali yaliyojitokeza nchini hivi karibuni, yakiwemo ya kubadilishwa kwa matokeo ya mtihani wa somo la Maarifa ya Uislamu na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA). 



Umati wa Waislamu ukiwa ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam leo, ukifuatilia na kusikiliza maneno yaliyokuwa yakizungumzwa na viongozi wao, wakati wa mkutano wa uzinduzi wa Kitabu cha maoni ya Waislamu cha mchakato Maoni ya Katiba mpya na kujadili masuala mbalimbali yaliyojitokeza nchini hivi karibuni. 

No comments:

Post a Comment