Waombolezaji wakiwa wamejipanga foleni tayari kwenda kutuoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa marehemu Willy Edward.
Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, marehemu Willy Edward, likiwa limefungwa kamba tayari kushushwa kaburini, wakati wa maziko yaliyofanyika nyumbani kwao Molotonga, Mugumu Mjini, wilayani Serengeti, Mkoa wa Mara leo.
Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, marehemu Willy Edward, likiingizwa kaburini tayari kwa kuzikwa mwili wake, wakati wa maziko yaliyofanyika nyumbani kwao Molotonga, Mugumu Mjini leo.
Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, marehemu Willy Edward, likishushwa kaburini wakati wa maziko yaliyofanyika nyumbani kwao Molotonga, Mugumu Mjini, wilayani Serengeti, Mkoa wa Mara leo.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mara, Hilikia Omindo, akiiongoza familia ya marehemu Willy Edward kuweka udongo kwenye kaburi wakati wa maziko yake nyumbani kwao Mugumu leo.
Watoto wa marehemu Willy Edward, Colman na Careb, wakiweka shada la maua kwenye kaburi la baba yao.
Mdogo wa marehemu Willy Edward, Essey Ogunde (kushoto) na kaka yao, wakiweka shada la maua kwenye kaburi lake, wakati wa mazishi Mugumu leo.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mara, Hilikia Omindo (kushoto) na Askofu John Adiema wa Dayosisi ya Rorya wakiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Willy Edward. (Picha zote na Richard Mwaikenda)
No comments:
Post a Comment