Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza jambo na mmoja kati ya wajumbe wa Umoja wa Watanzania, waishio nchini Brazil, wakati alipokutana nao katika hafla ya chakula cha jioni na mazungumzo, iliyofanyika Hoteli ya Arena, Rio de Jeneiro, jana Juni 22, 2012.
Katibu wa Umoja huo, akisoma risala yao kwa Mhe. Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal wakati wa hafla hiyo jana.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza Viongozi wa Umoja wa Watanzania, waishio nchini Brazil, wakati alipokutana nao katika hafla ya chakula cha jioni na mazungumzo, iliyofanyika katika Hoteli ya Arena, Rio de Jeneiro, jana Juni 22, 2012. Kulia ni mke wa Makamu, Mama Zakhia Bilal, kushoto) ni Balozi wa Tanzania, nchini Brazil, Francis Malambugi.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mwenyekiti wa Umoja wa Watanzania, waishio nchini Brazil, Ally Abdula Faraji baada ya kumaliza hafla wakati alipokutana nao katika hafla hiyo fupi ya chakula cha jioni na mazungumzo, iliyofanyika katika hiyo, mjini Rio de Jeneiro, jana Juni 22, 2012. Kushoto ni Mke wa Makamu wa Rais, Mama Zakhia Bilal.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, mke wake, Mama Zakhia Bilal, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, Balozi wa Tanzania nchini Brazil, Francis Malambugi na Balozi Liberata Mulamula, wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Umoja wa Watazanaia, wakati alipokutana nao pamoja na Watanzania waishio nchini Brazil katika hafla ya chakula cha jioni na mazungumzo, iliyofanyika katika Hoteli ya Arena, Rio de Jeneiro, jana Juni 22, 2012. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR)
No comments:
Post a Comment