TANGAZO


Sunday, June 17, 2012

Kifo cha Willy Edward, nyumbani ni vilio na huzuni tuuu, Jambo Leo wafadhaishwa


 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts, inayochapisha Gazeti la Jambo Leo na jarida la Jambo Brand Tanzania, Juma Pinto (kushoto) na Mkurugenzi mwenza wa Kampuni hiyo, Benny Kisaka (wa pili), wakiwa kwenye msiba wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, marehemu Willy Edward Ogunde uliopo nyumbani kwa kaka wa marehemu Mburahati, Dar es Salaam leo asubuhi. Willy amefariki ghafla leo alfajiri mjini Morogoro alikokuwa akihudhuria semina ya siku moja ya masuala ya Sensa. Kutoka kulia ni ndugu zake marehemu, Dennis Ongiri, Joseph Rabach na Julius Rabach.


 Baadhi ya waandishi wa habari wa Gazeti la Jambo Leo na Jarida la Jambo Brand Tanzania, wakishiriki kwenye msiba wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, marehemu Willy Edward. Mwili wa marehemu Willy unasafirishwa mchana huu kutoka Morogoro kwenda kuhifadhiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam. Taratibu za mazishi zinaendelea kuratibiwa kwa ushirikiano wa ndungu na viongozi wa Jambo Concepts, lakini kwa mujibu wa kaka wa marehemu, Rabach, mazishi yatafanyika nyumbani kwao marehemu, mjini Mugumu Wilaya ya Serengeti, mkoani Mara. Siku ya mazishi itatangazwa baadaye.
                           Mjane wa marehemu Willy Edward, Rehema (katikati), akiwa kwenye majonzi.


 Mjane wa marehemu Willy Edward, Rehema akilia wakati wa msiba huo leo asubuhi.


 Waombolezaji wakimfariji mjane wa marehemu Willy Edward, Rehema.


Mke wa marehemu na jamaa wa karibu wakimwaga machozi kutokana na msiba huo.


Akina mama waombolezaji wakiwa na huzuni na wengine kumwaga machozi kwenye msiba huo.

 Mtangazaji wa TBC, Grace Kingarame akimfariji  mjane wa marehemu Willy Edward, Rehema.


 Mpiga picha wa TBC, Mary Hondo, akimfariji mjane wa marehemu, Rehema Edward. 


 Mtoto wa mwisho wa marehemu Willy Edward, Caren (2), akiwa na babake mkubwa, Dennis Rabach
                           Mtoto wa mwisho wa marehemu, Willy Edward, Caren akiwa nyumbani kwao kwenye msiba, Mburahati jijini Dar es Salaam leo.


 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts Limited, inayochapisha gazeti la Jambo Leo na jarida la Jambo Brand Tanzania, Juma Pinto akihojiwa na Grace Kingarame wa TBC katika msiba huo. (Picha zote na Kamanda wa Matukio)

No comments:

Post a Comment