TANGAZO


Sunday, June 17, 2012

Willy Edward Ogunde, ametutoka, hatunaye tena





Aliyekuwa Mhariri Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Willy Edward, ametutoka, hatunaye tena. Marehemu amefia mjini Morogoro alikokwenda kikazi, kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo ya Sensa ya watu kwa Wahariri wa vyombo vya Habari mjini humo na baada ya kuhudhuria mafunzo hayo, kabla ya kurudi jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo, umauti ukamkuta baada ya kupatwa shinikizo la damu kutokana na kubanwa na mbavu. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema Peponi, Amin. 


Hapa marehemu Willy Edward alipokuwa akishiriki masuala ya michezo wakati wa Kombe la NSSF, mwaka jana, timu ya Jambo Leo ilipokuwa ikichuana na TBC1, Uwanja wa Sigara Chang'ombe jijini Dar es Salaam na Jambo leo kuibuka na ushindi wa mabao 3-2.   



 Hapa akiwa kwenye tuzo za Taswa 2011, Diamond Jubilee jijini Juni 14, 2012.

 Mhariri Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Willy Edward (aliyekaa), akiwa na waandishi waandamizi wa vyombo mbalimbali katika hafla hiyo.

Hapa marehemu Willy Edward (kulia), akiwa na Rais Jakaya Kikwete wakati wa uhai wake. 



Marehemu Willy Edward (katikati), ambaye alikuwa Mhariri Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, akisikiliza maelekezo ya jinsi ya kujaza dodoso refu, litakalojazwa wakati wa sensa ya  watu na makazi inatarajia kufanyika kote nchini kuanzia tarehe 26, mwezi wa nane mwaka huu. Hii ndiyo semina yake ya mwisho aliyohudhuria Morogoro juzi na kisha kukutwa na umauti kabla ya kurudi jijini Dar es Salaam. Wahariri pamoja na waandishi waandamizi walihudhuria mkutano wa siku moja wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 iliyofanyika jana mjini Morogoro. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Usajili  Idara ya Habari Jamali  Zuberi. (Picha na Anna Nkinda - Maelezo)

No comments:

Post a Comment