TANGAZO


Sunday, June 17, 2012

Mwili wa marehemu Willy Edward ulipowasili Muhimbili kwa kuhifadhiwa


Baadhi ya waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari, wakiusubiri mwili wa marehemu Willy Edward, wakati ukiwasili Muhimbili jijini Dar es Salaa, jioni hii.
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Free Media, ambayo inachapidsha Magazeti ya Tanzania Daima na Sayari, Absalom Kibanda, akimpa pole Mkurugenzi wa Jambo Concepts, Juma Pinto kufuatia kifo cha Mhariri Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Willy Edward kilichotokea mkoani Morogoro usiku wa kuamkia leo. 
 Mkurugenzi wa Jambo Concepts, Juma Pinto  akilia kwa uchungu baada ya kuona gari lililokuwa limebeba mwili wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa Jambo Leo, marehemu Willy Edward likiingiza mwili wa marehemu katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar.
 Mhariri wa Gazeti la Tanzania Daima Jumapili, Salehe Mohamed (kushoto), Mhariri wa Habari wa Gazeti la Mtanzania, Kulwa Karedia, Mwandishi wa Michezo Tanzania Daima, Ruhazi Ruhazi na Frank Balile wa Gazeti la Super Star wakiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuusubiri mwili huo.


Mkurugenzi wa Jambo Concepts, Juma Pinto (kushoto), akiwa na baadhi ya wahariri na waandishi waandamizi wa habari, wakiushusha mwili wa marehemu Willy Edwad kwenye gari kwa ajili ya kwenda kuhifadhiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini leo jioni, mara baada ya kuwasili kutoka Morogoro.
 Mwili wa marehemu Willy Edward, ukiingizwa katika chumba cha kuhifadhia maiti.
Baadhi ya wafanyakazi wenzake, wakiwa Muhimbili wakati mwili wa marehemu Willy Edward ukihifadhiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

No comments:

Post a Comment