TANGAZO


Friday, June 15, 2012

Hafla ya utoaji wa Tuzo za Wanamichezo bora wa Taswa, Diamond Jubilee

 Mgeni rasmi katika utoaji wa tuzo za wanamichezo bora wa Chama cha Waandishi wa habari za michezo (Taswa), Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, akiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Juma Pinto (kulia), wakati akienda kukabidhi tuzo ya mchezaji bora wa jumla usiku wa kuamkia leo, Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. (Picha na Kassim Mbarouk)


Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Morogoro, Anthony Mtaka (kulia), akimkabidhi Tuzo ya mchezaji bora wa Chama cha Waandishi wa habari za Michezo (Taswa), kwa mpira wa miguu upande wa wanawake, Mwanahamis Athuman baada ya kutangazwa mshindi katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo, Diamond Jubilee, jijini usiku wa kuamkia leo.


Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa zamani wa timu ya Taifa, iliyofanikiwa kushiriki mashindano ya Kombe la Mataifa Huru ya Afrika mwaka 1980, mara baada ya kuwakabidhi tuzo za heshima katika hafla hiyo.


Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Zanzibar (ZBC), Omar Said Ameir, akikabidhi tuzo ya mchezaji bora wa Tanzania katika soka ya wanaume, Agrey Morris wakati wa hafla hiyo.



Mwenyekiti wa Taswa, Juma Pinto, akimkabidhi tuzo ya Chama hicho, mchezaji bora wa kike kwa upande wa mpira wa Netibol, Lilian Singoni.


Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari za Michezo Tanzania (TASWA), Juma Pinto, akizungumza wakati wa hafla ya kutoa Tuzo za wachezaji bora wa Chama hicho, Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo. 


Mgeni rasmi, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, akizungumza katika hafla hiyo, wakati akitoa nasaha zake kwa wanamichezo, Vyama vya Michezo na taasisi mbalimbali za michezo kwenye hafla hiyo.


Mmoja wa Wakurugenzi wa Gazeti la Jambo Leo, Beny Kisaka (kushoto), akibadilishana mawazo na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Ridhwan Kikwete, wakati wa hafla hiyo.


Meneja Masoko wa Kampuni ya tsn, David Apiyo, akimkabidhi msaada Mpigapicha Mkuu wa Magazeti ya Daily/Sunday News, Athuman Hamis (kushoto), katika hafla hiyo baada ya kuguswa na matatizo yanayomwandama. Aliyesimama kushoto ni Mwenyekiti wa Taswa, Juma Pinto.


Mgeni rasmi, Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi (kushoto), akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya utoaji wa tuzo za wanamichezo bora wa Taswa, Masoud Sanani (kulia) na Mwenyekiti wa Taswa, Juma Pinto (katikati), wakati wa utoaji wa tuzo hizo usiku wa kuamkia leo.



Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa na Coastal Union, Salim Waziri (kulia), akimkabidhi tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa mpira wa miguu nchini, Shomari Kapombe, ambaye baadaye aliibuka mchezaji bora wa jumla katika tuzo hizo za Taswa na kuabidhiwa tuzo pamoja na sh. milioni 12 na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi.

 Mtangazaji wa Radio One na ITV, Isaac Muyenjwa wa Gamba, akitabasamu kwenye hafla hiyo.


 Mhariri Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Willy Edward (aliyekaa), akiwa na waandishi waandamizi wa vyombo mbalimbali katika hafla hiyo.


 Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), wakiwa na wadau wa michezo, Jamal Rwambo (wa pili kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Godfrey Nyange 'Kaburu' kwenye hafla hiyo ya utoaji tuzo.


Baadhi ya waandishi waandamizi na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari, wakipiga picha za kumbukumbu katika hafla hiyo, huku Mhariri wa Michezo wa Jambo Leo, Julus Kihampa (kushoto), akikata kiu kwa kinywaji.

 Kukundi la wanenguaji wa bendi ya Extra Bongo, wakimwaga mashoo ya nguvu ukumbini hapo wakati wa utoaji wa tuzo hizo. 


 Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya utoaji wa tuzo hizo, wakiwa jukwaani kujitambulisha kwa wadau wa michezo waliokuwa wamehudhuria utoaji wa tuzo za Taswa, ukumbini humo usiku wa kuamkia leo.


Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Serengeti Breweries (SBL), Jaji mstaafu Mark Bomani, akitetea jambo na Meneja Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Teddy Mapunda, wakati wa hafla hiyo, ambayo Kampuni ya SBL ndio waliokuwa wadhamini wakuu wa tuzo hizo.


Mwandishi Mwandamizi wa Michezo wa Gazeti la Jambo Leo, Asha Kigundula akiwa na mume wake katika hafla hiyo.


Mhariri wa Michezo wa Gazeti la Mwananchi, Ibrahim Bakari, naye hakupenda raha hiyo aipate peke yake, bali aliamua naye kuwa na mama watoto wake, Mama Siam wakiangalia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakitendeka ukumbini humo hadi mwisho.

No comments:

Post a Comment