TANGAZO


Friday, June 15, 2012

Rais Shein afungua Madrasa Nurullah Kitope Unguja

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (kulia), akifuatana  Makamo wake wa Pili ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kitope, Balozi Seif Ali Iddi pamoja na viongozi wengine,  alipowasili katika Jengo la Madrasat Nurullah Kitope, kwa ajili ya kulifungua rasmi, jingo lililojengwa kwa ufadhili wa Abdallwa Khamas na Mohamed Saidi, chini usimamizi  wa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua pazia kama  ishara ya ufunguzi wa madrasat Nurullah Kitope Zanzibar, iliyopo Wilaya ya Kaskazini B Unguja, Mkoa wa  Kaskazini. Kulia ni Makamo wake wa Pili, ambaye pia Mwakilishi wa Jimbo la Kitope, Balozi Seif Ali Iddi. Jengo hilo limejengwa kwa ufadhili wa Abdallwa Khamas na Mohamed Saidi, chini usimamizi wa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),  Mohamed Raza.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (katikati), akitembelea katika vyumba mbalimbali vya Madrasat Nurullah, Iliyopo  Kitope Wilaya ya Kaskazini B, Unguja mara baada ya kuifungua rasmi leo, akiongozwa na kiongozi wa
Madrasa hiyo, Mwalimu Juma Mohamed. Jengo la madrasa hiyo, limejengwa kwa Ufadhili wa Abdalla Khamas na Mohamed Saidi, chini usimamizi  wa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza.

Baadhi ya wanafunzi wa Kiume wa Madrasat Nurullah ya Kitope wakiwa mbele ya uwanja wa jengo la Madrasa yao, baada ya kufunguliwa rasmi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein leo. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (wapili kushoto), akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Pembe Juma Pembe (kushoto), wakati sherehe za ufunguzi wa Madrasat Nurullah ya Kitope, Wilaya ya Kaskazini B Unguja leo. Katikati ni Makamo wake wa  Pili ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kitope, Balozi Seif Ali Iddi na Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza (wa pili kulia).

Baadhi ya wanafunzi wa kike wa Madrasat Nurullah ya Kitope, wakiwa katika sherehe ya ufunguzi wa madrasa yao, iliyojengwa kwa kiwango cha hali ya juu, ambacho kitawaongezea  arizaidi ya kusoma kwa bidii, madrasa iliyofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, iliyojengwa kwa ufadhili wa Abdalla Khamas na Mohamed Saidi, chini usimamizi  wa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza.          


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ALhaj Dk.Ali Mohamed Shein, (wapili kushoto) akipokea risala ya wananchi na wanamadrasat   Nurullah ya Kitope Wilaya ya Kaskazini B Unguja,kutoka kwa Mwalimu Juma Mohamed,baada ya kuifungua Madrasa hiyo
jana, iliyojengwa na Abdalla Khamas na Mohamed Saidi, chini usimamizi wa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza. (Picha zote na Ramadhan Othman Ikulu)

No comments:

Post a Comment